Timu Zilizofuzu Robo Fainali EURO 2024
Wakati michuano ya UEFA EURO ikiendelea katika hatua ya 16 bora ambapo timu za mataifa 16 zinawania tiketi za kufuzu katika hatua ya robo fainali ya EURO 2024 ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 5/07/2024 ikihusisha bingwa wa Match 39 v Winner Match 37, mchezo ambao utachezeka Stuttgart – 12pm. Hapa tumekuletea orodha ya timu ambazo zimeweza kufuzu hatua ya robo fainali EURO 2024 na kujieka karika katika kubeba ubiongwa wa soka barani Ulaya.
Timu Zilizofuzu Robo Fainali EURO 2024
Robo fainali za Euro 2024 ni hatua muhimu ambapo ndoto za timu za kushinda kombe maarufu la Ubingwa wa Ulaya huanza kuonekana vizuri. Kuanzia hatua ya 16 bora, michuano hii inakuwa ya mtoano ambapo mshindi anaendelea mbele na aliyeshindwa anarejea nyumbani.
Njia za kufuzu zinaweza kuwa rahisi au ngumu kulingana na nafasi ambazo timu zilimaliza katika makundi yao, lakini kufikia hatua hii, kila timu iliyobaki ina matumaini makubwa ya kushinda na kusonga hadi hatua ya fainali. Kama ilivyo kwa hatua ya 16 bora, mechi za robo fainali zimepangwa tayari, na timu zinaingia kulingana na nafasi zao katika makundi.
Zifuatazo hapa chini ni timu ambazo zimefuzu hatua ya robofainali ya EURO 2024 baada ya kushinda michezo yao ya hatua ya 16 bora.
1. Ujerumani (Germany)
Ujerumani imefuzu kwa kishindo hatua ya robo fainali ya EURO 2024 baada ya kuitandika Denmark mabao 2-0 katika mchuano mkali uliochezwa Dortmund mnamo tarehe 29 Juni.
2. Uswisi (Switzerland)
Uswisi nao wamejihakikishia nafasi katika robo fainali kwa kuiondosha Italia, mabingwa watetezi, kwa ushindi wa mabao 2-0. Italia walishindwa kupenya ngome ya Uswisi na hivyo safari yao katika michuano hii imekwisha.
3. England
England iliifunga Slovakia na kusonga mbele kwenye robo fainali ya michuano ya EURO 2024 baada ya Jude Bellingham kufunga bao la ajabu la tikitaka katika dakika za jioni kabisa kabla ya mechi kumaliza, kuanzisha safari ya ushindi kwa kushinda mchezo uo kwa 2-1 baada ya muda wa ziada katika uwanja wa Arena AufSchalke huko Gelsenkirchen.
Ratiba ya Robo Fainali EURO 2024
Robo Fainali za EURO 2024 zinaanza tarehe 5 Julai 2024, kwa michezo miwili ya kusisimua:
- Mechi ya 45: Mshindi wa Mechi ya 39 atapambana na mshindi wa Mechi ya 37 mjini Stuttgart kuanzia saa 6 mchana.
- Mechi ya 46: Mshindi wa Mechi ya 41 atakabiliana na mshindi wa Mechi ya 42 jijini Hamburg kuanzia saa 9 alasiri.
Siku inayofuata, tarehe 6 Julai, kutakuwa na michezo mingine miwili:
- Mechi ya 47: Mshindi wa Mechi ya 43 atamenyana na mshindi wa Mechi ya 44 jijini Berlin kuanzia saa 9 alasiri.
- Mechi ya 48: Mshindi wa Mechi ya 40 atachuana na Uswisi mjini Dusseldorf kuanzia saa 6 mchana.
Kumbuka kuwa timu zitakazoshiriki katika kila mechi zitathibitishwa baada ya kukamilika kwa mechi za hatua ya 16 bora.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti