Tuzo za CAF 2025 Kutolewa Leo Saa 3 Usiku Katika Hafla Kubwa Rabat Morocco

Tuzo za CAF 2025 Kutolewa Leo Saa 3 Usiku Katika Hafla Kubwa Rabat Morocco

Sherehe ya utoaji wa tuzo za Shirikisho la Soka Afrika inatarajiwa kufanyika leo jijini Rabat nchini Morocco kuanzia saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki, katika tukio ambalo limepewa uzito mkubwa barani.

Huku mashindano yakiwa makali, tathmini kubwa inafanywa kwenye tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika, ambayo inawaniwa na Achraf Hakimi wa Paris Saint-Germain, Victor Osimhen wa Galatasaray na Mohamed Salah wa Liverpool. Hakimi ndiye pekee kati yao ambaye hajawahi kutwaa tuzo hiyo, licha ya kumaliza kwenye nafasi ya juu katika miaka miwili iliyopita.

Kwa upande wa mchezaji bora wa ndani barani Afrika, majina matatu ndiyo yapo kwenye hatua ya mwisho: Fiston Mayele wa Pyramids FC na timu ya taifa ya DR Congo, Oussama Lamlioui wa RS Berkane pamoja na beki wa Morocco na Pyramids Mohamed Chibi. Hawa wameingia kwenye orodha ya fainali kutokana na mafanikio yao katika michuano ya ndani na ile ya CAF msimu uliopita.

Hafla Kufanyika Rabat, Morocco

Sherehe ya Tuzo za CAF 2025 inatarajiwa kuanza saa 1:00 jioni kwa saa za Morocco (saa 3:00 usiku EAT) katika Ukumbi wa Mohamed VI Polytechnic University jijini Rabat. Tukio hili limepangwa kufanyika leo Jumatano, tarehe 19 Novemba 2025.

Waandaaji wamewathibitisha msanii wa Benin Angélique Kidjo na mchekeshaji wa Morocco Oualass kuwa watakaongoza hafla hiyo. Ratiba ya usiku huo pia inatazamiwa kujumuisha burudani za muziki kutoka kwa Douaa Lahyaoui wa Morocco, Awilo Longomba wa DR Congo na Fuse ODG kutoka Ghana.

Salah, Osimhen na Hakimi Katika Fainali ya Tuzo Kuu

Katika mashindano ya wanaume, usiku wa leo utatoa majibu ya nani ataibuka na tuzo ya juu barani Afrika. Achraf Hakimi, Mohamed Salah na Victor Osimhen ndiyo majina matatu yaliyobakishwa kwenye kitengo hicho. Haya ndiyo majina yaliyoongoza mjadala kwenye ulimwengu wa soka huku kila mmoja akitajwa kuwa na nafasi kutokana na michango yao katika klabu na timu za taifa.

Upande wa wanawake nao uko kwenye hatua ya mwisho. Wachezaji watatu walioteuliwa ni Ghizlaine Chebbak wa Al Hilal, Sanaa Mssoudy wa AS FAR pamoja na Rasheedat Ajibade wa Paris Saint-Germain.

Kwa ujumla, jumla ya tuzo 12 zinatarajiwa kutolewa katika usiku huu wa Tuzo za CAF 2025.

Jinsi ya Kutazama Tuzo za CAF 2025 Mubashara

Tuzo hizi kuruka mbashara kupitia AzamSports1HD kuanzia saa 3:00 usiku Pia zitarushwa live kupitia chaneli ya YouTube ya CAF.

Tuzo za CAF 2025 Kutolewa Leo Saa 3 Usiku Katika Hafla Kubwa Rabat Morocco

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Pantev Aandaa Mbinu Kali za kuizamisha Petro de Luanda Ligi ya Mabingwa Afrika
  2. Hat-Trick za Fernandes na Neves Zaipeleka Ureno Kombe la Dunia Baada ya Kuichapa Armenia 9-1
  3. Lyon Karibu Kumsajili Endrick Kutoka Real Madrid
  4. Wachezaji wa Simba Walioitwa Timu za Taifa November 2025
  5. Matokeo ya Yanga vs KMC Leo 09/11/2025
  6. Ratiba ya Yanga Klabu Bingwa 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo