Viingilio Mechi ya Yanga Vs Simba 25/06/2025

Viingilio Mechi ya Yanga Vs Simba 25/06/2025

Timu ya Wananchi Yanga SC itakutana na watani wao wa jadi Simba SC katika mchezo wa kukata na shoka utakaochezwa siku ya Jumatano tarehe 25 Juni 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Hii ni Dabi ya Kariakoo inayotazamwa kama ya kihistoria kutokana na ushindani uliopo kati ya timu hizi mbili, na hasa kutokana na mazingira ya msimu huu wa ligi ambayo yamekuwa ya mvutano mkubwa.

Mechi hii ni ya kiporo cha Ligi Kuu Bara, ambayo awali iliahirishwa mara mbili – Machi 8 na Juni 15 – na sasa imepangwa kuchezwa rasmi Juni 25, 2025. Hii ni mechi ya mwisho kwa msimu huu na itatumika kuamua bingwa wa Ligi Kuu kwa msimu wa 2024/2025.

Kaulimbiu ya “HATUCHEZI” iliyotawala mitandao ya kijamii na mtaa wa Bongo kabla ya kuamuliwa rasmi tarehe ya mchezo huu, imeacha gumzo kubwa. Awali, mashabiki wa Yanga walitangaza wazi kuwa hawatacheza mechi ya marudiano na Simba, lakini uamuzi wa mwisho umefanyika na sasa mpambano unatarajiwa kuwa wa aina yake.

Kwa sasa, Yanga SC inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 79, ikifuatiwa kwa karibu na Simba SC yenye pointi 78, kila timu ikiwa imecheza mechi 29. Hii ina maana kuwa tofauti ya pointi moja tu ndiyo inawatenganisha miamba hao wa soka Tanzania Bara.

Kwa upande wa Yanga, ushindi au sare kwenye mchezo huu utatosha kuwapa taji la ubingwa kwa mara ya nne mfululizo. Lakini kwa Simba, ni ushindi pekee ndio utakaoweka kombe mikononi mwao, jambo linaloongeza presha na msisimko wa mchezo huu wa Dabi ya kihistoria.

Viingilio Vya Mechi ya Yanga Vs Simba 25/06/2025

Kwa mujibu wa tangazo rasmi, viingilio vya mechi hiyo vimegawanyika kama ifuatavyo:

  • Mzunguko – TZS 5,000
  • Orange – TZS 10,000
  • VIP C – TZS 20,000
  • VIP B – TZS 30,000
  • VIP A – TZS 50,000 (Tayari zimeuzwa zote – Sold Out)
Viingilio Mechi ya Yanga Vs Simba 25/06/2025
Viingilio Mechi ya Yanga Vs Simba 25/06/2025

Viingilio hivi vimetolewa kwa lengo la kuwapa mashabiki wa aina zote nafasi ya kushuhudia pambano hili kubwa ambalo linaweza kuamua bingwa wa ligi kwa msimu huu.

Maandalizi ya Mechi na Msimamo wa Klabu

Kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mwisho, kikosi cha Yanga kilifanya kikao kizito huko Zanzibar kikihusisha wachezaji, benchi la ufundi, na viongozi wa juu wa klabu hiyo. Mkutano huo uliweka bayana dhamira ya klabu hiyo kuhakikisha ushindi au sare, na mastaa wa timu hiyo walitoa msimamo wao kuwa wako tayari kwa vita hiyo ya heshima.

Afisa mmoja mwandamizi wa Yanga alinukuliwa akisema:

“Tuna kikosi imara ambacho kinaweza kutupa matokeo tunayoyataka. Kuna matokeo mawili tu – kushinda au sare. Tunataka ushindi kwenye mechi hii kwa sababu imebeba heshima ya mashabiki wetu na viongozi wa timu.”

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mechi ya Yanga vs Simba Kupigwa Chini ya Uangalizi wa Waamuzi Kutoka Misri
  2. Tetesi Za Usajili Simba Leo 2025/2026
  3. Tetesi Za Usajili Yanga Leo 2025/2026
  4. Ratiba ya Mechi za Leo Ligi Kuu ya NBC 22/06/2025
  5. TFF Yafunga Rasmi Zoezi la Uchukuaji wa Fomu za Uongozi – Wagombea 25 Wajitokeza
  6. Tanzania Yashinda Ubingwa wa CECAFA Wanawake 2025 Kupitia Twiga Stars
  7. KMKM Mabingwa wa FA Cup Zanzibar 2025 Baada ya Ushindi wa 4-2 Dhidi ya Chipukizi
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo