Vituo Vya Tiketi Mechi ya Yanga Vs Simba 25/06/2025
Timu ya Wananchi Yanga SC itakutana na watani wao wa jadi Simba SC katika mchezo wa kukata na shoka hapo Jumatano ya tarehe 25 Juni 2025, katika dimba la Benjamin Mkapa Stadium, jijini Dar es Salaam. Hii ni mechi ya kiporo ya Ligi Kuu Bara ambayo ilikuwa imeahirishwa mara mbili—awali Machi 8, na baadaye Juni 15, kabla ya kuthibitishwa rasmi kuchezwa tarehe hiyo muhimu ya Juni 25, 2025.
Dabi hii ya Kariakoo si tu inahitimisha msimu wa NBC Premier League 2024/2025, bali pia ndiyo mechi inayotajwa kuwa ya kuamua bingwa wa msimu huu. Yanga SC inaongoza ligi kwa pointi 79, ikifuatiwa na Simba SC yenye alama 78, tofauti ya pointi moja tu ikiwatenganisha. Ushindi au sare kwa Yanga SC itamaanisha taji la nne mfululizo, wakati Simba SC watalazimika kushinda ili kutwaa ubingwa.
Katika hali ya maandalizi ya mechi hii kubwa, uongozi wa Yanga SC ulifanya kikao kizito Zanzibar pamoja na wachezaji wao, walimu na viongozi wa juu wa klabu hiyo. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kuhakikisha kuwa timu inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na ari, umoja na malengo ya kushinda kwa ajili ya mashabiki na heshima ya klabu.
Vituo Vya Tiketi Mechi ya Yanga Vs Simba 25/06/2025
Ili kurahisisha upatikanaji wa tiketi kwa mashabiki wote, vituo mbalimbali vimepangwa katika maeneo tofauti ya Dar es Salaam, Geita, na mikoa mingine. Mashabiki wanashauriwa kununua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu siku ya mechi.
- Young Africans – Jangwani
- Vunja Bei – Dar es Salaam Shops
- T-Money Ltd – Kigamboni
- Gitano Samweli – Mbagala Zakiem
- Khalfan Mohamed – Ilala
- Karoshy Pamba – Dar Live {Zakheim}
- Antonio Service – Sinza, Kivukoni
- Sovereign – Kinondoni Makaburini
- View Blue Skyline – Mikocheni
- Mkaluka Traders – Machinga Complex
- New Tech General Traders – Ubungo
- Duka la J5 Lingerie – Sinza kwa Remmy
- Mtemba Service Co – Temeke
- Jackson Kimambo – Ubungo
- Alphan Hinga – Ubungo
- Shirima Shop – Leaders
- Juma Burrah – Msimbazi
- Juma Burrah – Kivukoni
- Lampard Electronics – Geita
- Godwin Fredy – Geita
- Twisty Investment – Geita
- Gwambina Lounge – Gwambina
- Tumpe Kamwela – Kigamboni
- Sabana Business – Mbagala Maji Matitu
- Maduka yote ya TTCL Tanzania nzima
Maandalizi ya Mwisho kwa Vikosi
Kwa upande wa Yanga, kikosi kilirejea jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu kwa maandalizi ya mwisho. Mkutano wa ndani ulifanyika ukihusisha wachezaji, benchi la ufundi na uongozi mkuu wa klabu ambapo msisitizo uliwekwa kwenye umuhimu wa ushindi kama njia ya kulinda heshima ya klabu na mashabiki wake. “Tumezungumza nao kwa uwazi kuhusu uzito wa mchezo huu. Tunahitaji matokeo ya ushindi au sare, hakuna chaguo jingine,” alieleza mmoja wa viongozi.
Wachezaji nao walionesha utayari wa dhati kwa kuahidi kupambana hadi dakika ya mwisho ili kuwapa furaha mashabiki wa Yanga.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Mechi ya Yanga vs Simba Kupigwa Chini ya Uangalizi wa Waamuzi Kutoka Misri
- Tetesi Za Usajili Simba Leo 2025/2026
- Tetesi Za Usajili Yanga Leo 2025/2026
- Ratiba ya Mechi za Leo Ligi Kuu ya NBC 22/06/2025
- TFF Yafunga Rasmi Zoezi la Uchukuaji wa Fomu za Uongozi – Wagombea 25 Wajitokeza
- Tanzania Yashinda Ubingwa wa CECAFA Wanawake 2025 Kupitia Twiga Stars
- KMKM Mabingwa wa FA Cup Zanzibar 2025 Baada ya Ushindi wa 4-2 Dhidi ya Chipukizi
Leave a Reply