Viwanja Vitakavyo Tumika Mechi za Ligi Kuu 2024/2025
Msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, maarufu kama NBC Premier League, kwa mwaka 2024/2025 unakaribia kuanza rasmi mnamo Agosti 16, 2024. Mashabiki wa soka kote nchini wanatazamia msimu huu mpya kwa hamu, huku viwanja mbalimbali vikiwa tayari kwa mapambano ya kumtafuta bingwa wa soka Tanzania kwa msimu wa 2024/2025.
Katika makala hii, tumekuletea viwanja 12 ambavyo vimeidhinishwa kutumika kwa mechi za ligi kuu msimu huu.
Orodha Kamili ya Viwanja
Kwa sasa, viwanja 12 vimeidhinishwa rasmi kutumika katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara:
- KMC Complex, Dar es Salaam: Uwanja huu utakuwa mwenyeji wa mechi za KMC FC, Simba SC, na Coastal Union FC.
- Azam Complex, Dar es Salaam: Azam FC na Yanga SC watatumia uwanja huu kama uwanja wao wa nyumbani.
- Sokoine Stadium, Mbeya: KenGold FC na Tanzania Prisons FC watacheza mechi zao za nyumbani hapa.
- Lake Tanganyika, Kigoma: Mashujaa FC watatumia uwanja huu kama uwanja wao wa nyumbani.
- CCM Kirumba, Mwanza: Pamba Jiji FC watacheza mechi zao za nyumbani hapa.
- Majaliwa Stadium, Lindi: Namungo FC watatumia uwanja huu kama uwanja wao wa nyumbani.
- Kaitaba Stadium, Kagera: Kagera Sugar FC watacheza mechi zao za nyumbani hapa.
- Meja Isamuhyo, Dar es Salaam: JKT Tanzania watatumia uwanja huu kama uwanja wao wa nyumbani.
- Ali Hassan Mwinyi, Tabora: Tabora United FC watacheza mechi zao za nyumbani hapa.
- Tanzanite, Manyara: Fountain Gate FC watatumia uwanja huu kama uwanja wao wa nyumbani.
- CCM Liti, Singida: Singida Black Stars FC watacheza mechi zao za nyumbani hapa.
- Jamhuri Stadium, Dodoma: Dodoma Jiji FC watatumia uwanja huu kama uwanja wao wa nyumbani.
Uwanja Utakao Tumiwa na Timu Nyingi
Katika msimu huu, KMC Complex utakuwa uwanja wenye shughuli nyingi zaidi, ukiwa mwenyeji wa mechi za timu tatu: KMC FC, Simba SC, na Coastal Union FC.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Mzize Amtaja Chama Kuwa na Jicho la Pasi
- Liverpool Imechukua EPL Mara Ngapi
- Bingwa Wa Ngao ya Jamii 2024 ni Yanga Sc, Yailaza Azam FC 4-1 Katika Fainali
- Simba Warudi Sokoni Kusaka Mshambuliaji Mpya Kuongeza Makali
- Tanzania Yamaliza Olimpiki 2024 Mikono Mitupu
- Matokeo ya Simba Vs Coastal union Leo Ngao ya Jamii 11/08/2024
Weka Komenti