Wachezaji Walio Ongeza Mkataba Simba 2024/2025 | Wahcezaji Waliopewa Mikataba mipya Simba
Wakati klabu ya Simba ikiendelea na zoezi la kutoa Thank you kwa wachezaji ambao hawajakidhi ubora na matarajio ya klabu kwa msimu ulipita ambao haukua bora kwa Simba, Wapo wachezaji ambao Simba imeanza kuwapa mikataba mipya ambayo itawabakiza katika klabu kwa msimu unaokuja wa 2024/2025. Hadi sasa orodha ya wahezaji walio Ongeza mkataba Simba imejazwa na majina makubwa ya wachezaji wazawa ambao walionesha kiwango kikubwa licha ya kabu kuwa na msimu mbovu.
Mashabiki wa Simba wanaweza kutarajia kuona sura nyingi zinazozoeleka msimu ujao, huku klabu ikiendelea kufanya usajili wa kimkakati kuimarisha safu zote za kikosi. Mabadiliko haya yanatarajiwa kuleta ushindani mkali zaidi ndani ya kikosi na kuongeza ari ya kupambania mataji katika msimu wa 2024/2025. Hapa tutakuletea wachezaji wote ambao wametangazwa kuongezwa mkataba na Simba Sc.
Wachezaji Walio Ongeza Mkataba Simba 2024/2025
Simba SC imefanya jitihada za kuimarisha kikosi chao kwa kusaini mikataba mipya na wachezaji muhimu, ikiwemo:
- Mzamiru Yasin Selemba
- Kibu Denis Prosper
- Israel Patrick Mwenda
Mzamiru Yasin Selemba
Klabu ya Simba Sc imethibitisha kumsainisha kiungo, Mzamiru Yasin Selemba nyongeza ya mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kusalia klabuni hapo mpaka 2026.
Mkataba wa awali wa Mzamiru (28) aliyejiunga na Simba mnamo Julai 1, 2016 ulitamatika mwishoni mwa msimu uliopita
Kibu Denis Prosper
Klabu ya Simba SC imefanikiwa kumbakisha kiungo mshambuliaji wao Kibu Denis Prosper (25) almaharufu kama Kibu Mkandaji, baada ya kumpa kandarasi mpya ya miaka miwili baada ya mkataba wake wa awali kutamatika.
Kibu ambaye alijiunga na klabu ya Simba SC akitokea Mbaye city amekuwa na mchango mkubwa kwenye klabu hiyo huku akiwa na uwezo wa kushanmbulia na kuzuia licha ya msimu huu mambo kumuendea Kombo.
Kuelekea msimu mpya Kibu atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaotetea nembo ya Simba SC Kitaifa na kimataifa.
“Kibu D ataendelea kusalia klabuni baada ya kuongeza mkataba mpya” imesema taarifa ya Simba Sc kwenye mitandao ya kijamii.
Israel Patrick Mwenda
Mlinzi wa Simba, Israel Patrick Mwenda amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia katika kikosi cha Simba.
Kwa mara ya kwanza Mwenda alijiunga na Simba Julai, 2021 akitokea KMC.
Mapendekezo Ya Mhariri:
- Taarifa Rasmi: Simba Yatangaza Kuachana na Henock Inonga
- Tuisila Kisinda Atajwa Kutakiwa Coastal Union 2024/2025
- Kikosi Cha Simba 2024/2025 | Wachezaji Wote wa Simba
- Wachezaji walioachwa na Simba 2024/2025
- Simba SC Yachagua Ismailia, Misri Kwa Kambi Ya Kujiandaa Na Msimu Mpya
- Tetesi za Usajili simba 2024/2025
Weka Komenti