Wachezaji Wanaowania Tuzo za TFF 2024/2025

Wachezaji Wanaowania Tuzo za TFF 2024/2025

Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa msimu wa 2024/2025 zinatarajiwa kufanyika tarehe 5 Desemba 2025 katika ukumbi wa The Super Dome jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo kubwa inakusudia kutambua na kuheshimu mchango wa wachezaji, benchi la ufundi, waamuzi na wadau mbalimbali waliotoa mchango muhimu katika soka la Tanzania msimu mzima.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya TFF, tuzo zimegawanywa katika makundi makuu matano:

  1. Tuzo za Ligi Kuu NBC
  2. Tuzo za Kombe la Shirikisho la CRDB
  3. Tuzo za Ligi Kuu ya Wanawake
  4. Tuzo za Ligi Nyingine
  5. Tuzo za Utawala

Msimu huu pia utaweka historia mpya kwa kutoa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Tanzania Anayecheza Nje – Upande wa Wanawake, tuzo ambayo ilianzishwa msimu wa 2023/24 lakini ilitolewa kwa upande wa wanaume pekee. Uongezwaji huu umeonekana kama hatua muhimu katika kuimarisha usawa na kutambua mchango wa wanamichezo wa kike katika soka la kimataifa.

Wanaowania Tuzo za Ligi Kuu ya NBC 2024/2025

Wachezaji Wanaowania Tuzo za TFF 2024/2025

Mchezaji Bora – Ligi Kuu NBC

Kundi hili limejumuisha wachezaji waliotoa mchango mkubwa kwa timu zao msimu uliopita. Miongoni mwao ni mastaa kutoka klabu tatu kubwa nchini.

  • Dickson Nickson Job – Young Africans SC (Tanzania)
  • Feisal Salum Abdallah – Azam FC (Tanzania)
  • Jean Charles Ahoua – Simba SC (Ivory Coast)
  • Max Nzengeli – Young Africans SC (RDC Congo)
  • Peodoh Pacome Zouzoua – Young Africans SC (Ivory Coast)

Uteuzi huu umeakisi ubora wa wachezaji waliokuwa na mchango mkubwa katika mbio za ubingwa msimu wa 2024/2025.

Kipa Bora – Ligi Kuu NBC

Katika nafasi ya mlinda mlango, majina matatu yametajwa:

  • Djigui Diara – Young Africans
  • Moussa Camara – Simba SC
  • Patrick Evans Munthali – Mashujaa FC

Kiungo Bora – Ligi Kuu NBC

  • Feisal Salum Abdallah – Azam FC
  • Jean Charles Ahoua – Simba SC
  • Peodoh Pacome Zouzoua – Young Africans

Beki Bora – Ligi Kuu NBC

  • Antony Urbain Tra Bi – Singida Black Stars
  • Dickson Nickson Job – Young Africans
  • Lusajo Elukaga Mwaikenda – Azam FC

Chipukizi Bora

  • Anthony Richard Mligo – Namungo FC
  • Bakari Msimu – Coastal Union
  • Berno Halfan Ngassa – Tanzania Prisons

Wanaowania Tuzo za Kombe la Shirikisho la CRDB

Mchezaji Bora – Kombe la CRDB

  • Stephane Aziz Ki – Young Africans
  • Clement Mzize – Young Africans
  • Emmanuel Keyekeh – Singida Black Stars

Wanaowania Tuzo za Ligi Kuu ya Wanawake

Katika Ligi Kuu ya Wanawake, ushindani umeonekana kuwa mkubwa, hasa kutoka timu za JKT Queens, Yanga Princess, Simba Queens na Bunda Queens.

Mchezaji Bora – Wanawake

  • Donisia Minja – JKT Queens
  • Esther Maseke – Bunda Queens
  • Jeannine Mukandayisenga – Yanga Princess
  • Jentrix Shikangwa – Simba Queens
  • Stumai Abdallah – JKT Queens

Kipa Bora – Wanawake

  • Asha Mrisho – Mashujaa Queens
  • Najlat Abbas – JKT Queens
  • Rita Akarekor – Yanga Princess

Chipukizi Bora – Wanawake

  • Elizabeth Chenge – JKT Queens
  • Elizabeth Joseph – Alliance Girls
  • Esther Maseke – Bunda Queens

Kocha Bora – Wanawake

  • Edna Lema – Yanga Princess
  • Esther Chabruma – JKT Queens
  • Yusuf Basigi – Simba Queens

Mfungaji Bora – Wanawake

  • Stumai Abdallah – JKT Tanzania

Tuzo za Ligi Nyingine

Mchezaji Bora Ligi ya U-20

  • Ashraf Kibeku – Azam FC
  • Luqman Mbala – Kagera Sugar
  • Popah Mwatomdoa – Kongolo FC

Mchezaji Bora – Tanzania Anayecheza Nje (Wanaume)

  • Mbwana Samatta – Ugiriki
  • Novatus Dismas – Uturuki
  • Simon Msuva – Iraq

Mchezaji Bora – Tanzania Anayecheza Nje (Wanawake)

Tuzo mpya msimu huu kwa upande wa wanawake inawania na:

  • Diana Lucas – Trabzon (Uturuki)
  • Enekia Kasonga – Mazatlan (Mexico)
  • Opa Clement – FC Juarez (Mexico)

Mchezaji Bora – Ligi ya Championship

  • Andrea Albert Simchimwa – Geita Gold
  • Mwani Willy Thobias – Mbeya City
  • Razin Hafidh Haji – Mtibwa Sugar

Mchezaji Bora – First League

  • George Elwin Komba – Rhino Rangers
  • Moses Peter Kitandu – Rhino Rangers
  • Ramadhani Hashimu Kalanje – Tanesco SC

Tuzo za Utawala

Tuzo hizi zitatangazwa moja kwa moja wakati wa hafla ya Desemba 5.

  • Mchezaji Gwiji
  • Tuzo ya Heshima Soka la Wanawake
  • Tuzo ya Rais
  • Tuzo ya Heshima

Waamuzi na Benchi la Ufundi

Mwamuzi Bora

  • Ahmed Arajiga – Manyara
  • Saad Mrope – Dar es Salaam
  • Abdallah Mwinyimkuu – Singida

Mwamuzi Msaidizi Bora

  • Hamdani Saidi – Mtwara
  • Kassim Mpanga – Dar es Salaam
  • Zaneth Balamba – Iringa

Kocha Bora – Ligi Kuu

  • Ahmad Ally – JKT Tanzania
  • Fadlu Davids – Simba SC
  • Rachid Taoussi – Azam FC

Timu Yenye Nidhamu

  • Kagera Sugar
  • KMC FC
  • Namungo FC

Zaidi ya tuzo 40 zinatarajiwa kutolewa katika hafla ya mwaka huu, ikionyesha ukubwa na umuhimu wa tukio hili kwa maendeleo ya soka nchini. Kwa mujibu wa TFF, uchaguzi wa wachezaji na makocha unaolenga kutambua ubora, nidhamu, na mchango wao katika kukuza mchezo wa mpira wa miguu. Kwa mashabiki na wadau wa michezo, orodha hii imeongeza hamasa kuelekea Desemba 5, ambapo washindi wa Wachezaji Wanaowania Tuzo za TFF 2024/2025 watatangazwa rasmi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Simba SC Yatambulisha Jezi Mpya Kwa Ajili ya Mechi za CAF 2025/2026
  2. Tuzo za CAF 2025 Kutolewa Leo Saa 3 Usiku Katika Hafla Kubwa Rabat Morocco
  3. Jezi Mpya za Yanga za Ligi ya Mabingwa Afrika CAF 2025/2026
  4. Kikosi cha Yanga Chawasili Zanzibar Kujiandaa na Mchezo wa AS FAR Rabat
  5. Kariakoo Dabi Yapigwa Kalenda Kutoka Desemba 13 Hadi Machi Mwakani
  6. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mikoa Yote (NECTA PSLE Results)
  7. Pantev Aandaa Mbinu Kali za kuizamisha Petro de Luanda Ligi ya Mabingwa Afrika
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo