Wallace Karia Abaki Bila Mpinzani Baada ya Wagombea Watano Kuenguliwa

Wallace Karia Abaki Bila Mpinzani Baada ya Wagombea Watano Kuenguliwa

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewatoa kwenye mchakato wa uchaguzi wagombea watano wa nafasi ya urais, na kumwacha Wallace Karia kuwa mgombea pekee anayetetea kiti hicho katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Kiomoni Kibamba, imeelezwa kuwa kati ya wagombea sita waliowasilisha fomu za kugombea urais, ni mgombea mmoja tu Wallace Karia aliyekidhi vigezo vyote vya kikanuni. Kibamba alibainisha kuwa wagombea wanne walishindwa kutimiza masharti ya msingi ya uchaguzi, huku mgombea mmoja akishindwa kufika kwenye usaili.

“Kwenye nafasi ya urais kulikuwa na wagombea sita. Mmoja hakufika kwenye usaili na wanne hawakukidhi matakwa ya kikanuni. Mgombea mmoja pekee ametimiza matakwa yote, na huyo ni Wallace Karia,” alisema Wakili Kibamba.

Wallace Karia Abaki Bila Mpinzani Baada ya Wagombea Watano Kuenguliwa

Mchakato wa Usaili wa Wagombea Urais TFF

Kamati ya Uchaguzi ilifanya kazi ya kuchambua na kuhakiki sifa za wagombea wote kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa TFF. Katika mchakato huo, wagombea waliopitishwa walipaswa kuonyesha uthibitisho wa vigezo mbalimbali vilivyowekwa na shirikisho hilo.

Kutokana na tathmini hiyo, wagombea waliokatwa walionekana kukosa sifa za msingi au kushindwa kuhudhuria usaili, jambo lililopelekea kuondolewa kwenye mchakato.

Majina ya wagombea wote waliowasilisha nia ya kugombea nafasi ya urais ni Wallace Karia, Richard Shija, Mshindo Msolwa, Ally Mayai, Mustapha Himba, na Ally Thabit Mbingo. Kati yao, ni Karia pekee aliyefuzu hatua zote.

Haki ya Rufaa Kwa Walioenguliwa

Licha ya kuenguliwa, Kamati ya Uchaguzi imesisitiza kuwa wagombea waliokatwa bado wanayo nafasi ya kukata rufaa. Kibamba alisema kuwa iwapo mgombea yeyote anahisi hajatendewa haki, ana siku sita za kuwasilisha rufaa kwa Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi.

“Sisi ni binadamu, inawezekana wapo wanaohisi wameonewa. Wanayo nafasi ya kwenda kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi. Tukirudishiwa jina la mgombea, sisi hatuna shida, tutalipokea na kuendelea na mchakato,” aliongeza.

Kamati hiyo imesisitiza kuwa itaendelea kusubiri orodha rasmi kutoka Kamati ya Rufaa kabla ya kuendelea na hatua zinazofuata za uchaguzi.

Katika nafasi nyingine kama ujumbe wa kamati, jumla ya wagombea 19 waliwasilisha fomu, ambapo 17 walihudhuria usaili. Kati ya hao, 10 walipitishwa na saba wakakatwa kutokana na kukosa sifa zinazotakiwa. Zoezi la uchaguzi litaendelea mara baada ya Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi kutoa uamuzi wake kuhusu rufaa zitakazowasilishwa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ibenge Atua Tanzania Kujiunga Rasmi na Azam FC kwa Msimu wa 2025/26
  2. Tetesi Za Usajili Yanga Leo 2025/2026
  3. Tetesi Za Usajili Simba Leo 2025/2026
  4. Makombe ya Yanga 2024/2025
  5. Florent Ibenge Aaga Rasmi Al Hilal Sudan, Aelekea Kujiunga na Azam FC
  6. Lionel Messi anukia Ligi Kuu ya Uingereza EPL
  7. Miloud Hamdi Ajiunga na Ismaily ya Misri Baada ya Kuipa Yanga Mataji 3
  8. Simba SC Yapiga Hesabu Kumnasa Balla Moussa Conte Kutoka Sfaxien
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo