Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Kwanza 2026

Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Kwanza 2026

Wanafunzi 937,581, sawa na asilimia 100 ya wote wenye sifa, wameteuliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2026 na tayari wamepangiwa shule za Serikali nchini. Hawa ni wanafunzi waliofanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2025, ambapo walipata kati ya alama 121 hadi 300, kiwango kilichowastahili kuendelea na elimu ya sekondari.

Akitoa taarifa hii Desemba 4, 2025, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe, alibainisha kuwa uchaguzi wa wanafunzi kuingia Kidato cha Kwanza 2026 umefanyika kwa kuzingatia miongozo ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Alisisitiza kuwa kila mwanafunzi mwenye ufaulu unaokidhi vigezo amepewa nafasi katika shule za Serikali, akisema:

“Kila mtahiniwa aliyefanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2025 na kupata jumla ya alama 121 hadi 300 amechaguliwa na kupangiwa shule ya Serikali.”

Taarifa hii imezidi kuthibitisha dhamira ya Serikali kuhakikisha kuwa hakuna mwanafunzi anayekosa nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari, sambamba na utekelezaji wa sera ya elimu msingi bila malipo.

Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Kwanza 2026

Idadi ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Kwanza 2026

Uchaguzi wa wanafunzi kwa mwaka 2026 umehusisha jumla ya 937,581 waliofaulu na kukamilisha mchakato wa upangaji wa shule. Kati yao:

  • Wasichana: 508,477
  • Wavulana: 429,104
  • Wenye mahitaji maalum: 3,228
  • Wasichana: 1,544
  • Wavulana: 1,684

Wanafunzi hawa wamepangwa katika jumla ya shule 5,230 za sekondari za Serikali, hatua ambayo inadhihirisha upanuzi mkubwa wa miundombinu ya elimu nchini.

Profesa Shemdoe alitoa msisitizo maalum kwa kundi la wanafunzi wenye mahitaji maalum, akieleza kuwa maandalizi yamefanyika kuhakikisha wanapata mazingira stahiki ya kujifunzia.

ANGALIA Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato Cha Kwanza 2026

Bofya Jina la Mkoa ambako ipo shule uliyosoma kuangalia majina yote

ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA
GEITA IRINGA KAGERA
KATAVI KIGOMA KILIMANJARO
LINDI MANYARA MARA
MBEYA MOROGORO MTWARA
MWANZA NJOMBE PWANI
RUKWA RUVUMA SHINYANGA
SIMIYU SINGIDA SONGWE
TABORA TANGA

Uteuzi wa Wanafunzi Katika Shule Maalum na Shule za Ufaulu wa Juu

Serikali imeendelea kuendeleza utaratibu wa kuwapangia wanafunzi wenye ufaulu wa juu katika shule zenye rekodi bora kitaaluma. Kwa mwaka 2026:

1. Shule za Ufaulu wa Juu (Special Schools)

Jumla ya 815 wamechaguliwa kujiunga na shule hizi, wakiwemo:

  • Wasichana: 335
  • Wavulana: 480

Shule hizo ni pamoja na: Ilboru, Msalato, Kibaha, Kilakala, Mzumbe, Tabora Boys, na Tabora Girls – ambazo zinajulikana kwa kuandaa wanafunzi katika ushindani mkubwa kitaaluma.

2. Shule za Amali za Bweni

  • Wanafunzi: 3,411
  • Wasichana: 1,279
  • Wavulana: 2,162

3. Shule za Bweni za Kitaifa

  • Wanafunzi: 7,360
  • Wasichana: 5,014
  • Wavulana: 2,346

4. Shule za Kutwa

Idadi kubwa ya wanafunzi wamepangiwa shule za kutwa:

  • Jumla: 925,065
  • Wasichana: 501,849
  • Wavulana: 424,116

Hizi ni shule zinazopokea wanafunzi wanaoishi maeneo jirani na shule, hatua inayolenga kupunguza changamoto za usafiri na gharama kwa wazazi.

Mikakati ya Serikali Kuhakikisha Wanafunzi Wote Wanaanza Masomo Kwa Wakati

Serikali imeweka mikakati mahususi kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliochaguliwa wanajiunga Kidato cha Kwanza bila vikwazo. Profesa Shemdoe alisema kuwa maandalizi yamefanyika mapema ili kuhakikisha shule zote zinakuwa tayari Januari 2026.

“Wanafunzi wote waliochaguliwa wataanza muhula wa kwanza tarehe 13 Januari 2026. Nawaasa watumie fursa waliyoipata kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao.”

Aliongeza kuwa uongozi wa mikoa, wilaya, na halmashauri una jukumu muhimu kuhakikisha kuwa:

  • Wanafunzi wanaripoti shuleni kwa wakati
  • Wanafunzi wanaandikishwa bila kuchelewa
  • Hakuna mwanafunzi anayekosa masomo kwa sababu ya vikwazo vya kifamilia au kijamii
  • Maandalizi ya miundombinu, walimu, na mitaala mipya yanakamilishwa kwa wakati

Katika mkazo wake, Profesa Shemdoe aliwakumbusha wazazi umuhimu wa ushirikiano, akisema:

“Ninawahimiza wazazi, walezi na jamii kushirikiana na uongozi wa shule ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata haki yake ya msingi ya elimu na kubaki shuleni hadi atakapohitimu.”

Utekelezaji wa Mtaala Mpya na Kipindi cha Orientation

Serikali pia imeelekeza kuwa shule zote zitumie ipasavyo kipindi cha orientation, ambacho ni muhimu katika:

  • Kuwawezesha wanafunzi kuimarisha ujuzi wa mawasiliano katika Kiingereza
  • Kuwajengea uwezo wa kuchagua fani wanazopendelea katika shule zenye mkondo wa amali
  • Kuwandaa kwa mabadiliko ya mtaala mpya ulioanza kutumika Januari 2024

Mwongozo huu unalenga kuwasaidia wanafunzi kuanza safari ya elimu ya sekondari wakiwa na msingi imara na kuelewa madhumuni ya kila kozi watakayosoma.

Wito kwa Uongozi wa Shule na Halmashauri Nchini

Katika kuhakikisha utekelezaji wa sera ya Elimu Bila Malipo, viongozi wote kuanzia ngazi ya mkoa hadi shule wamesisitizwa kutimiza majukumu yao. Waziri aliwaelekeza:

  • Wakuu wa shule kuhakikisha mazingira ni rafiki kwa wanafunzi wapya
  • Mamlaka za mikoa na wilaya kusimamia kikamilifu uandikishaji
  • Halmashauri kuhakikisha vifaa muhimu vinapatikana kwa wakati
  • Jamii kushirikiana katika kutokomeza utoro na changamoto nyinginezo

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2026
  2. Form One Selection 2026 | Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza 2026
  3. Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA
  4. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 (PSLE)
  5. Kidato cha Nne Kuanza Mitihani ya Taifa Kesho November 17 2025
  6. NECTA Standard Seven Results 2025 Released: 81.8% of Candidates Pass the PSLE Examination
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo