Wasanii Watakao Tumbuiza Simba Day 2024
Tamasha la Simba Day 2024 linalosubiriwa kwa hamu kubwa na maelfu ya masahabiki wa Simba Tanzania na nje ya Tanzania kufanyika hapo kesho Agosti 3 katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es salaam. Katika tamasha hili, Mashabiki wa Simba watashuhudia utambulisho wa wachezaji wote wa Simba waliosajiliwa na wale waliobakizwa kuelekea msimu wa 2024/2025.
Nje na utambulisho, Tamasha hili limetajwa kuhusisha burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki na hapa Habariforum tumekuletea orodha kamili ya wasanii watakao sherehesha katika tamasha hili.
Orodha ya Wasanii Watakao Tumbuiza Simba Day 2024
- Ali Kiba
- Joh Makini
- Dulla Makabila
- Chino
Mbali na wasanii, pia kutakua na Madj nguli wa kimataifa wakinogesha sherehe hii maarufu kama Simba Day 2024. Kwenye mashine atakuwepo Dj Bike, Dj White na Dj Sinyorita.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti