Washindi Tuzo Za Baraza La Michezo Tanzania BMT 2024

Washindi Tuzo Za Baraza La Michezo Tanzania BMT 2024

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) leo Juni 1, 2025, limetangaza rasmi washindi wa tuzo mbalimbali za michezo nchini Tanzania katika hafla ya aina yake iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Super Dome, Masaki – Dar es Salaam.

Hafla hiyo ya kihistoria ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wanamichezo na wadau wa michezo, huku ikilenga kuwaenzi Watanzania walioleta heshima kwa taifa kupitia mashindano ya kimataifa.

Katika tukio hilo muhimu, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ndiye mlezi mkuu wa sekta ya michezo nchini.

Waziri Mkuu aliwasilisha ujumbe wa Rais pamoja na kupokea tuzo maalum kwa niaba yake, ikiwa ni kutambua mchango wa Dkt. Samia katika kukuza na kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini.

Washindi Tuzo Za Baraza La Michezo Tanzania BMT 2024

Lengo la Tuzo za BMT

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi. Neema Msita, lengo kuu la tuzo hizi ni kuwaenzi na kuwatambua Watanzania wote wanaoiwakilisha nchi kimataifa kupitia michezo mbalimbali, na kwa kufanya hivyo, kuliinua jina la Tanzania kwenye anga za kimataifa kwa maslahi ya taifa na maendeleo ya mtu mmoja mmoja.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa alisisitiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuendeleza sekta ya michezo. Alibainisha kuwa michezo si tu burudani, bali ni nyenzo muhimu ya afya, mshikamano wa kitaifa, ajira, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Katika kutambua mchango wake binafsi, Waziri Mkuu pia alikabidhiwa tuzo ya heshima kutokana na juhudi zake katika kusimamia na kuhamasisha maendeleo ya michezo nchini.

Washindi wa Tuzo za Michezo BMT 2024

Katika hafla hiyo, washindi kutoka makundi mbalimbali ya michezo walitangazwa rasmi na kupokea tuzo zao mbele ya viongozi, wadau na mashabiki wa michezo:

1. Timu Bora ya Mwaka 2024 – Wanaume

Yanga SC: Klabu hii kongwe imeibuka mshindi wa tuzo ya timu bora ya mwaka, baada ya kuibwaga timu pinzani kutoka mchezo wa kikapu, Dar City Basketball Club.

2. Mwanamichezo Bora wa Kiume kutoka Shuleni

Baraka Sanjigwa: Ameibuka mshindi kutoka mchezo wa riadha kwa upande wa wanafunzi wa shule, akionyesha vipaji vya hali ya juu na uzalendo.

3. Mwanamichezo Bora wa Kike kutoka Shuleni

Neema Hamis: Mchezaji wa netiboli aliyeibuka na tuzo hii kutokana na mchango wake mkubwa na nidhamu ya hali ya juu katika mchezo huo.

4. Mwanamichezo Bora Kijana wa Kike

Namnyaki Isaya: Nyota chipukizi wa mpira wa kikapu ambaye amepata tuzo kutokana na uwezo wake wa kipekee na mchango wake kwenye timu za vijana.

5. Mwanamichezo Nguli wa Zamani

Teresa Dismas: Bingwa wa zamani wa mchezo wa riadha ambaye ametunukiwa tuzo ya heshima. Tuzo hiyo ilipokelewa kwa niaba yake na Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Evelyn Nyamka.

6. Mwandishi Bora wa Michezo – Wanawake

Fatma Chikawe (Azam Media): Mwanahabari mwenye weledi ambaye ameshinda tuzo ya mwandishi bora wa michezo kwa upande wa wanawake kwa mwaka 2024 kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia ya habari za michezo nchini.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Hawa Apa Maofisa wa Mechi ya Nusu Fainali CRDB Bank Federation Cup 2024/2025
  2. Kikosi cha Taifa Stars kilichoitwa kambini Kuelekea COSAFA na Mechi ya Kirafiki
  3. Coastal Union Yapiga Hesabu Kali Kumchukua Anicet Kiazayidi
  4. Chelsea Yaipiga Bao Manchester United Usajili wa Liam Rory Delap
  5. Xabi Alonso Aahidi Kurejesha Ufalme wa Real Madrid
  6. Singida BS Yashindwa Kutamba Mbele ya Simba Ligi Kuu NBC
  7. Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria 2025 – Pakua PDF Hapa!
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo