Wiliete Sc Vs Yanga Leo 19/09/2025 Saa Ngapi?

Wiliete Sc Vs Yanga Leo 19/09/2025 Saa Ngapi?

Hatimaye pazia la mashindano ya kimataifa kwa ngazi ya klabu barani Afrika linafunguliwa rasmi leo. Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania, Young Africans SC (Yanga SC), wanashuka dimbani kuanza safari yao ya kupeperusha bendera ya Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika almaharufu kama CAF Chmapions League. Mchezo huu wa kwanza unawakutanisha mabingwa wa Tanzania na Wiliete Sports Clube ya Angola, hatua ya awali ya mashindano hayo makubwa.

Wiliete Sc Vs Yanga Leo 19/09/2025 Saa Ngapi?

Mashabiki wengi wamekuwa wakijiuliza kwa hamu kubwa, “Wiliete Sc Vs Yanga leo 19/09/2025 saa ngapi?” Jibu ni kwamba mchezo huu wa kimataifa utapigwa majira ya saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Wiliete Sc Vs Yanga Leo 19/09/2025 Saa Ngapi?

Kwa wapenzi wa soka walioko Tanzania, ni muda mzuri kushuhudia pambano hili kubwa ambalo litakuwa na ushindani wa hali ya juu kati ya mabingwa wa Tanzania na wenyeji kutoka Angola. Mchezo wa Wiliete Sc Vs Yanga leo utafanyika katika uwanja mkubwa na wa kisasa wa Estádio 11 de Novembro, uliopo Luanda, Angola. Uwanja huu una historia ya kuwa mwenyeji wa mechi kubwa za kimataifa, jambo linaloongeza hadhi ya mchezo huu muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Mechi za CAF Leo 19 September 2025
  2. Gamondi Atamba na Singida BS Baada ya Kutwaa Ubingwa wa Haraka
  3. Ratiba ya Mechi za Leo 18 September 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo