Wydad Casablanca Yafungashiwa Virago Kombe la Dunia Bila Pointi

Wydad Casablanca Yafungashiwa Virago Kombe la Dunia Bila Pointi

Washington D.C, Marekani – Klabu ya Wydad Casablanca kutoka Morocco imemaliza safari yake katika mashindano ya Kombe la Dunia la Klabu 2025 kwa namna ya kusikitisha, baada ya kuondolewa katika hatua ya makundi bila kuvuna pointi hata moja.

Michuano hiyo ambayo inaendelea kutimua vumbi jijini Washington D.C, Marekani, imeshuhudia Wydad ikiwa timu pekee kutoka Afrika iliyoshindwa kuambulia hata sare kwenye mechi zake zote tatu.

Hali hiyo imeifanya Wydad Casablanca kufungashiwa virago mapema, na kurejea nyumbani ikiwa na rekodi isiyopendeza, tofauti na wawakilishi wengine wa Afrika walioweza kupata angalau ushindi au sare katika hatua hiyo ya makundi.

Katika mchezo wao wa mwisho wa kundi G, Wydad walikabiliana na Al Ain kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu kwenye dimba la Audi Field, Washington D.C. Mshambuliaji wao mahiri Cassius Mailula aliwapa matumaini mapema baada ya kufunga bao dakika ya 4, akiunganisha pasi murua ya Mohamed Moufid.

Hata hivyo, matumaini hayo yalidumu kwa muda mfupi baada ya Al Ain kusawazisha dakika za lala salama kabla ya mapumziko kupitia mkwaju wa penalti uliotokana na faulo aliyofanyiwa Adis Jasic ndani ya eneo la hatari.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kutoka kwa Al Ain, na ndani ya dakika tano tu, waliongeza bao la pili lililowekwa kimiani na Kaku, aliyemalizia pasi safi kutoka kwa Matias Palacios, na kufanya mambo kuwa magumu zaidi kwa Wydad Casablanca.

Wydad Casablanca Yafungashiwa Virago Kombe la Dunia Bila Pointi

Wydad Casablanca Yamaliza Bila Pointi – Afrika Yawakilishwa Vizuri na Wengine

Wydad sasa imeandika historia ya aina yake – lakini kwa upande wa aibu – kwa kuwa klabu pekee kutoka Afrika kushindwa kupata pointi yoyote kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Dunia la Klabu 2025.

Kwa kulinganisha, klabu zingine za Afrika ziliweza kujitahidi na kupata angalau matokeo ya heshima:

  1. Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) waliongoza kwa pointi 4
  2. Esperance de Tunis (Tunisia) walijizolea pointi 3
  3. Al Ahly (Misri) walitoka na pointi 2

Wydad, kwa upande wao, walimaliza mkiani katika kundi lao, wakiwa na mabao machache na matokeo mabaya zaidi ukilinganisha na wawakilishi wenzao wa Afrika.

Michuano Yaendelea kwa Hatua ya Mtoano

Wakati Wydad Casablanca ikirejea nyumbani kwa masikitiko, michuano ya Kombe la Dunia la Klabu 2025 inaingia katika hatua ya mtoano, huku vigogo wa soka duniani wakisubiriwa kuchuana vikali. Miongoni mwa michezo inayosubiriwa kwa hamu ni kama ifuatavyo:

  • Manchester City vs Al Hilal
  • Real Madrid vs Juventus
  • Paris Saint-Germain vs Inter Miami
  • Benfica vs Chelsea
  • Palmeiras vs Botafogo
  • Flamengo vs Bayern Munich
  • Inter Milan vs Fluminense
  • Borussia Dortmund vs Monterrey

Hatua hiyo ya mtoano itaanza rasmi tarehe 28 Juni 2025, ambapo mashabiki wa soka duniani wataendelea kushuhudia burudani ya hali ya juu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Milos Kerkez Ajiunga Rasmi na Liverpool kwa Ada ya Pauni Milioni 40
  2. Christian Eriksen Aondoka Man United Baada ya Utumishi wa Miaka Mitatu
  3. Kikosi cha Tanzania CHAN 2024: Wachezaji Kuingia Kambini Julai 7, 2025
  4. Yanga Yailaza Simba 2-0 na Kutwaa Kombe la Ligi Kuu Kwa Mara ya 31
  5. Vituo Vya Tiketi Mechi ya Yanga Vs Simba 25/06/2025
  6. Mechi ya Yanga vs Simba Kupigwa Chini ya Uangalizi wa Waamuzi Kutoka Misri
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo