Yanga SC vs Tanzania Prisons Leo 04/04/2026 Saa Ngapi?

Yanga SC vs Tanzania Prisons Leo 04/04/2026 Saa Ngapi?

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, leo watakuwa dimbani kuendeleza mbio za kutetea taji lao, wakikabiliana na Tanzania Prisons katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Mashabiki wengi wamekuwa wakijiuliza, Yanga SC vs Tanzania Prisons leo 04/04/2026 saa ngapi? ambapo pambano hili litaanza majira ya saa 12:30 jioni.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC utapigwa katika Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge, jijini Dar es Salaam, ukiwakutanisha vigogo hawa wawili wakiwa katika hali ya uhitaji mkubwa wa matokeo.

Yanga SC vs Tanzania Prisons Leo 04/04/2026 Saa Ngapi?

Yanga SC kwenye presha licha ya rekodi bora

Licha ya kuwa kileleni mwa msimamo, Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa katika kipindi kigumu cha matokeo. Kikosi hicho kimepata sare tatu mfululizo katika michezo iliyopita, hali inayoongeza presha kwa benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Pedro Goncalves.

Katika mechi hizo:

  • Sare ya 0-0 dhidi ya Azam FC
  • Sare ya 0-0 dhidi ya TRA United
  • Sare ya 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar

Rekodi ya Yanga bado ni ya kuvutia kwani haijapoteza mechi yoyote katika michezo 36 ya Ligi Kuu Bara tangu Novemba 7, 2024, ilipofungwa mabao 3-1 na Tabora United (sasa TRA United).

Kwa msimu huu:

  • Mechi: 16
  • Ushindi: 11
  • Sare: 5
  • Pointi: 38

Kocha msaidizi wa Yanga, Matthew Silva, alieleza kuwa licha ya matokeo yasiyoridhisha ya hivi karibuni, timu hiyo imefanya maandalizi ya kutosha:

“Ni kweli tumepitia kipindi kigumu kwa mechi tatu zilizopita ambazo hatukupata ushindi… tutapambana ili kupata matokeo mazuri.”

Hata hivyo, Yanga itamkosa kipa wake Djigui Diarra ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu.

Tanzania Prisons wapambana kujiokoa

Kwa upande wa Tanzania Prisons, hali si shwari pia. Timu hiyo haijashinda mechi nne mfululizo tangu ilipopata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo FC Februari 14, 2026.

Katika michezo iliyofuata:

  • Imefungwa mechi tatu
  • Imetoka sare moja

Kwa msimu huu:

  • Mechi: 17
  • Ushindi: 3
  • Sare: 4
  • Kupoteza: 10
  • Nafasi: 15
  • Pointi: 13

Kocha wa sasa, Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’, ambaye alichukua nafasi hiyo Februari 27, 2026, bado hajapata ushindi katika mechi tatu alizoiongoza timu hiyo.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Nsajigwa alisema:

“Hatupo sehemu nzuri… tutacheza kwa nidhamu kubwa ya kujilinda, lakini wakati huohuo tukiwashambulia pia kwa kuwashtukiza.”

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Simba SC vs Coastal Union leo 02/04/2026
  2. Ratiba ya Mechi za Simba Sc Mwezi April 2026
  3. Makundi ya Kombe la Dunia 2026
  4. Tottenham Hotspur Yaachana na Igor Tudor Baada ya Mfululizo wa Matokeo Mabaya
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo