Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025 Saa Ngapi?

Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025 Saa Ngapi?

Timu ya Wananchi Yanga leo, Jumatano tarehe 24 Septemba 2025, inaanza rasmi safari ya kulitetea taji la Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Mchezo huo muhimu utafanyika katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo Yanga SC watakuwa wenyeji wa Pamba Jiji FC. Kwa mujibu wa ratiba ya mechi za leo 24/09/2025, pambano hili limepangwa kuchezwa kuanzia saa 1:00 usiku, likifuatiwa na mchezo mwingine wa ligi kati ya Azam FC na Mbeya City utakaopigwa saa 3:00 usiku katika Uwanja wa Azam Complex. Mashabiki watapata nafasi ya kufuatilia mechi zote moja kwa moja kupitia AzamSports1HD.

Taarifa Kuhusu Mechi

  • 🏆 #nbcpremierleague
  • 🆚 Pamba Jiji FC
  • 🗓️ 24 September 2025
  • 🏟️ Benjamin Mkapa
  • ⏱️ 1:00 Usiku

Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025 Saa Ngapi?

Hali za Timu Kabla ya Mchezo

Yanga SC inakutana na Pamba Jiji ikiwa na morali ya hali ya juu baada ya kuonyesha ubabe katika michezo miwili ya hivi karibuni. Mnamo Septemba 16, Wanajangwani waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba SC katika Ngao ya Jamii.

Aidha, walifunga ukurasa wa kimataifa kwa ushindi mnono wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Wiliete SC ya Angola kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, matokeo yaliyowapa zawadi ya shilingi milioni 15.

Kwa upande wa benchi la ufundi, kocha Romain Folz anatarajiwa kutumia uzoefu na mbinu alizoonesha kimataifa ili kuhakikisha Yanga inaanza kampeni ya ligi kwa ushindi. Hii ni mechi yake ya kwanza ndani ya ligi msimu huu akiwa kocha mkuu wa Wananchi.

Pamba Jiji, chini ya kocha Francis Baraza, wamesalia na changamoto ya kuimarisha safu yao ya ulinzi. Katika mchezo wao wa kwanza wa ligi msimu huu walitoka sare ya 1-1 na Namungo FC ugenini. Licha ya kupata bao la kuongoza dakika ya 19 kupitia Staphan Siwa, walishindwa kulinda ushindi na kuruhusu goli la kusawazisha dakika ya 90+7 kupitia Abdulaziz Shahame.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Fadlu Davids Atambulishwa Kama Kocha Mkuu wa Raja Casablanca ya Morocco
  2. Lamine Yamal Abeba Tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo wa Mwaka (Kopa Trophy)
  3. Simba Yamtambulisha Hemed Suleiman Kama Kocha wa Mpito
  4. Ousmane Dembélé Ashinda Tuzo ya Ballon d’Or 2025
  5. Ratiba ya Mechi za Leo 22/09/2025
  6. Matokeo ya Gaborone United vs Simba leo 20/09/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo