Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025 Fainali ya CRDB Saa Ngapi?

Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025 Fainali ya CRDB Saa Ngapi?

Timu ya Wananchi Yanga SC leo itashuka tena dimbani kulitetea taji la Kombe la CRDB Federation Cup, baada ya kuhitimisha rasmi kampeni ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC siku ya Jumatano tarehe 25 Juni kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Simba SC. Katika mwendelezo wa mafanikio yao msimu huu, Yanga SC inatarajiwa kushuka dimbani usiku huu wa leo tarehe 29 Juni 2025 kuikabili timu ngumu ya Singida Black Stars katika fainali ya CRDB Federation Cup.

Mchezo huu wa fainali ya kombe la CRDB Federation Cup almaharufu kama kombe la FA Tanzania utatimua kivumbi katika Uwanja wa New Amaan, Zanzibar, na saa rasmi ya kuanza ni saa 2:15 usiku.

Yanga vs Singida Black Stars Leo 29/06/2025 Fainali ya CRDB Saa Ngapi?

Viingilio vya Mchezo

Kwa mashabiki wanaotarajia kushuhudia pambano hili la kukata na shoka, viingilio vimetangazwa rasmi kama ifuatavyo:

  • VIP – Tsh 20,000
  • Urusi – Tsh 10,000
  • Orbit & Saa – Tsh 5,000

Mashabiki wote wanaaswa kununua tiketi zao mapema kutokana na umuhimu wa mchezo huu na mvuto mkubwa uliopo baina ya timu hizi mbili.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Fainali ya CRDB Federation Cup 2025
  2. Chelsea Yajipanga Kuzima Moto wa Di Maria Katika Mechi ya Usiku Dhidi ya Benfica
  3. Simba Yavizia Saini ya Issa Fofana Nchini Ivory Coast Kama Mrithi wa Camara
  4. Ratiba ya CHAN 2024/2025 | CAF African Nations Championship
  5. Ratiba ya Kombe la Dunia la Vilabu 2025 Hatua ya 16 Bora
  6. Form Five Selection 2025: Majina Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 Yatangazwa!
  7. Timu Zilizofuzu Hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia la Vilabu 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo