Yanga VS TMA Star Leo 11/04/2026 Saa Ngapi?

Yanga VS TMA Star Leo 11/04/2026 Saa Ngapi?

Timu ya wananchi Young Africans Sports Club (Yanga SC) leo inashuka dimbani kuendelea na harakati za kutetea ubingwa wake katika michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB, huku ikikabiliana na wapinzani wao TMA Stars katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mashabiki wengi wamekuwa wakitafuta kujua: Yanga vs TMA Star leo 11/04/2026 saa ngapi? Hapa chini kuna kila kitu unachohitaji kufahamu kuhusu pambano hilo muhimu.

⏰ Yanga vs TMA Stars Leo Saa Ngapi?

  • 📅 Tarehe: 11 Aprili 2026
  • 🏟️ Uwanja: KMC Complex Stadium
  • ⏱️ Muda: Saa 12:30 Jioni

Angalia Hapa Kikosi cha Yanga VS TMA Star Leo 11/04/2026

Huu ni mchezo wa hatua ya 16 bora (knockout), ambapo mshindi atasonga mbele moja kwa moja.

Yanga VS TMA Star Leo 11/04/2026 Saa Ngapi?

Yanga inaingia na Kasi Kubwa Kombe la CRDB

Yanga inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na morali ya juu baada ya ushindi mkubwa wa mabao 7-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika hatua ya awali. Katika mchezo huo, mshambuliaji Laurindo Aurelio aliibuka shujaa kwa kufunga hat-trick yake ya kwanza msimu huu.

Kocha wa Yanga, Pedro Goncalves, ameonyesha wazi kuwa timu yake ina nia ya dhati ya kulinda taji hilo, akiwatumia nyota wake muhimu hata kwenye michezo ya mtoano.

Kwa upande wa TMA Stars, timu hiyo inayofundishwa na Omary Matiko imeonyesha ushindani mkubwa baada ya kuiondoa Prisons kwa ushindi wa bao 1-0. Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji Ernest Baltazari, ambaye anatajwa kuwa tishio kubwa kwa safu ya ulinzi ya Yanga.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ratiba ya Kombe la Shirikisho CRDB FA Cup Leo 10/04/2026
  2. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
  3. AFCON 2027 Kufanyika Mwezi Juni na Julai
  4. Harry Maguire Asaini Mkataba Mpya Manchester United Hadi 2027
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo