Yanga Yaangukia Kundi B na Al Ahly Droo ya Makundi Klabu Bingwa 2025/2026

Yanga Yaangukia Kundi B na Al Ahly Droo ya Makundi Klabu Bingwa 2025/2026

Droo ya hatua ya makundi ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League 2025/2026) imefanyika Jumatatu tarehe 3 Novemba 2025 jijini Johannesburg, Afrika Kusini, ikishuhudiwa na wakuu wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) na nyota wa zamani wa soka barani humo.

Katika droo hiyo iliyoendeshwa na Kiongozi wa Idara ya Mashindano ya CAF, Nassar Khaled, akisaidiwa na Alex Song (Cameroon) pamoja na Christopher Katongo (Zambia), Klabu ya Yanga SC imepangwa kwenye Kundi B, kundi ambalo limeonekana kuwa miongoni mwa magumu zaidi katika hatua hii ya mashindano.

Yanga Yaangukia Kundi B na Al Ahly Droo ya Makundi Klabu Bingwa 2025/2026

Yanga SC Kundi B na Miamba ya Afrika

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wameangukia Kundi B wakikabiliana na miamba mitatu kutoka Kaskazini mwa Afrika wakiwemo Al Ahly ya Misri, mabingwa mara 12 wa michuano hiyo, ASFAR ya Morocco, na JS Kabylie ya Algeria.

Kundi hili linatajwa kuwa miongoni mwa yale yenye ushindani mkubwa kutokana na historia na uzoefu wa timu hizo kwenye mashindano ya CAF Champions League. Kwa mujibu wa ratiba ya mashindano hayo, hatua ya makundi itaanza wiki ya tarehe 21–23 Novemba 2025, kabla ya kusimama kwa muda kupisha Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 zitakazofanyika nchini Morocco. Michuano ya makundi inatarajiwa kurejea tena wiki ya tarehe 23–25 Januari 2026, na kuendelea hadi Februari 2026.

Makundi Mengine ya CAF Champions League 2025/2026

Mbali na kundi la Yanga, droo hiyo pia imetangaza upangaji wa makundi mengine matatu kama ifuatavyo:

Kundi A: RS Berkane (Morocco), Pyramids FC (Misri), Rivers United FC (Nigeria), Power Dynamos FC (Zambia)

Kundi B: Al Ahly (Misri), Yanga SC (Tanzania), ASFAR (Morocco), JS Kabylie (Algeria)

Kundi C: Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Al Hilal SC (Sudan), MC Alger (Algeria), FC Lupopo (DR Congo)

Kundi D: Esperance de Sportive (Tunisia), Simba SC (Tanzania), Atletico Petroleos de Luanda (Angola), Stade Malien (Mali)

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Timu Zilizofuzu Makundi Kombe la Shirikisho Afrika CAF 2025/2026
  2. Timu Zilizofuzu Makundi Klabu Bingwa Afrika 2025/2026
  3. Matokeo ya Simba SC VS Nsingizini Leo 26/10/2025
  4. Cv ya Pedro Gonçalves Kocha Mpya wa Yanga Sc 2025/2026
  5. Yanga SC Yamtangaza Pedro Gonçalves Kama Kocha Mkuu Mpya wa Timu
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo