Yanga Yapata Ushindi Mzuri Dhidi ya Kagera Sugar, Mudathir Anafunga Bao La Pekee
Baada ya kukosekana kwenye ufungaji kwa muda, hatimaye Mudathir anatupia goli lililo watoa machozi Kagera Sugar baada ya kupambana kuzuia kwa muda wa dakika takribani 70. Zikiwa zimesalia dakika saba kabla ya kumalizika kwa mchezo, kiungo Mudathir Yahya aliyetokea benchi alifanikiwa kuleta vicheko kwenye mitaa ya Jangwani kwa kufunga bao pekee lililoipa ushindi timu ya Yanga dhidi ya Kagera Sugar.
Bao lililofungwa na Mudathir dakika ya 83 lilitokana na pasi ya Stéphane Aziz Ki, huku kiungo huyo akiwa na dakika 11 pekee tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya Pacôme Zouzoua. Ni katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania uliochezeka kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, ambapo ilionekana kipindi cha kwanza kumalizika kwa matokeo ya 0-0.
Mabadiliko kadhaa katika kipindi cha pili yaliamua mechi na kujihakikishia pointi tatu muhimu nyumbani baada ya mzunguko wa kwanza 0-0 dhidi ya Kagera Sugar. Ushindi huu unaendeleza harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC ambapo sasa tumefikisha pointi 68 baada ya kupoteza mara 26.
Hadidi sasa zimesalia mechi nne ili kuhitimisha msimu ambapo Yanga Sc wanahitaji pointi tano pekee ili kutetea ubingwa wa ligi kuu nchini Tanzania. Katika mechi nne zilizobaki, yanga Sc itacheza na Mtibwa Sugar (ugenini), Dodoma Jiji (ugenini), Tabora United (nyumbani) na Tanzania Prisons (nyumbani).
Machaguo Ya Mhariri:
Weka Komenti