Yanga Yatinga Raundi ya Pili CAF Champions League Baada ya Ushindi wa 2-0

Yanga Yatinga Raundi ya Pili CAF Champions League Baada ya Ushindi wa 2-0

Dar es Salaam, Septemba 27, 2025 – Ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Pacome Zouzoua na Aziz Andabwile kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Wiliete FC umeivusha Yanga SC hatua ya pili ya awali ya CAF Champions League 2025/26.

Kwa matokeo hayo, Yanga inafuzu kwa jumla ya mabao 5-0, ikijipatia faida kubwa kutokana na ushindi wa 3-0 ilioupata wiki iliyopita kwenye mchezo wa kwanza huko Angola.

Katika raundi inayofuata, Wanajangwani wanatarajiwa kuvaana na Silver Strikers ya Malawi, ambayo imepita hatua ya awali kwa faida ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya 1-1 kwenye mechi ya kwanza na kisha kulazimisha suluhu katika marudiano.

Mchezo ulianza kwa Yanga kuonekana kutokuwa katika ubora wao wa kawaida, wakikosa nafasi kadhaa ambazo zingeweza kufanikisha bao la mapema. Kufikia mapumziko, timu zote zilikuwa bado hazijafumania nyavu, na ubao wa matokeo ukisomeka 0-0.

Hata hivyo, kipindi cha pili kiligeuka kuwa na mwelekeo tofauti. Dakika ya 71, shujaa wa Wanajangwani Pacome Zouzoua alivunja ukimya baada ya kumalizia kwa ustadi pasi murua kutoka kwa Andy Boyeli, ambaye naye alikuwa amepokea mpira kutoka kwa Zouzoua nje kidogo ya boksi la adhabu la Wiliete. Bao hilo liliwasha shangwe kubwa kwa mashabiki waliokuwa wakijaza uwanja wa Mkapa.

Yanga Yatinga Raundi ya Pili CAF Champions League Baada ya Ushindi wa 2-0

Aziz Andabwile Afunga Pazia Dakika za Mwisho

Wakati mchezo ukielekea kumalizika, Yanga ilihakikisha ushindi wake dakika ya 87 kupitia kwa Aziz Andabwile. Kiungo huyo alifunga kwa kichwa baada ya kupokea kona safi iliyochongwa na Offen Chikola, na kufanya matokeo kuwa 2-0. Goli hilo liliua matumaini ya wapinzani na kuhitimisha ndoto za Wiliete kwenye safari ya mashindano haya.

Mlandege Waaga Mashindano

Kwa upande mwingine, mambo hayakuwa mazuri kwa wawakilishi wa Zanzibar, Mlandege SC, ambao licha ya ushindi wa 3-2 nyumbani dhidi ya Ethiopian Insurance, walishindwa kusonga mbele. Timu hiyo ya Ethiopia iliendelea kwa ushindi wa jumla wa 4-3, ikibebwa na ushindi wa awali wa 2-0 walioupata jijini Addis Ababa.

Nini Kinachofuata kwa Yanga?

Baada ya ushindi huu, Yanga sasa inaelekeza nguvu zake kwenye mchezo ujao dhidi ya Silver Strikers, ambapo ushindi utaikaribisha zaidi hatua ya makundi ya CAF Champions League 2025/26. Mashabiki wa Wanajangwani wanatarajia kuona mwendelezo wa ubabe wao barani Afrika, huku benchi la ufundi likiendelea kusisitiza nidhamu na maandalizi bora kuelekea michezo ijayo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025
  2. Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025 Saa Ngapi?
  3. Kikosi cha Yanga vs Wiliete SC Leo 27/09/2025
  4. KMKM Yatinga Raundi ya Pili ya CAF Baada ya Kuichapa AS Port ya Djibouti
  5. Sergio Busquets Atangaza Kustaafu Soka Mwishoni Mwa Msimu Huu
  6. Kocha Folz Aahidi Ushindi Mkubwa Mechi ya Marudiano Dhidi ya Wiliete
  7. Yanga SC Yazindua Jezi Mpya Ili Kulinda Mapato Dhidi ya Jezi Feki
  8. Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo