Yanga yazipiku Al Ahly na Sundowns katika Rekodi za Ulinzi

Yanga yazipiku Al Ahly na Sundowns katika Rekodi za Ulinzi

Mabeki wa kati wa Yanga SC, Dickson Job, Ibrahim Bacca, na Bakari Mwamnyeto, wamekuwa tegemeo kubwa katika safu ya ulinzi ya klabu hiyo kwa misimu mitatu mfululizo. Umahiri wao umewafanya siyo tu kuhodhi nafasi hizo ndani ya klabu, bali pia kuwa nyota katika timu ya taifa, Taifa Stars. Wachezaji hawa wamefanikiwa kuzuia wapinzani wengi huku rekodi zao zikivuka hata zile za klabu kubwa za Afrika kama Al Ahly ya Misri na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Yanga yazipiku Al Ahly na Sundowns katika Rekodi za Ulinzi

Katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita, mabeki hawa wameisaidia Yanga kuruhusu mabao machache mno—jumla ya mabao 40 katika mechi 90 za Ligi Kuu. Uwezo huo umeifanya klabu ya Yanga kuwa imara kiasi cha kutosajili mabeki wa kigeni katika nafasi hiyo, huku mabosi wa timu wakielekeza nguvu zaidi kwenye usajili wa wachezaji wa nafasi nyingine.

Kwa upande wa rekodi za ulinzi za mabeki wa Yanga, zinazidi hata zile za mabingwa wa Afrika. Mamelodi Sundowns kwa misimu mitatu iliyopita wameruhusu jumla ya mabao 44, wakati Al Ahly imeruhusu mabao 62 katika kipindi hicho. Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani mabeki wa Yanga wamefanikiwa kuimarisha ulinzi wa timu, na kufanya kuwa ngome ngumu kupenyeza kwa wapinzani.

Mafanikio haya yamejengwa kwenye msingi uliowekwa na mabeki wa kati wazawa waliowahi kutamba Yanga, kama Nadir Haroub ‘Cannavaro’, na Kelvin Yondani, ambao waliwaandaa kizazi hiki cha wachezaji kama Mwamnyeto kuendeleza ubora huo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Djuma Shabani atimkia Ufaransa
  2. Azam FC Yasaini Mkataba wa Ushirikiano na Klabu ya Uswidi
  3. Wydad Bado Katika Harakati za Kumsajili Mzize
  4. Kikosi cha Chelsea UEFA Conference League 2024/2025
  5. Bellingham Afuata Nyayo za Ronaldo, Aingia YouTube Rasmi
  6. Manchester United Yatangaza Kikosi cha Wachezaji 25 kwa Ajili ya Europa 2024-25
  7. Ufaransa Yashushiwa Kipigo cha Goli 3-1 na Itali
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo