Simba Yapewa Vitisho Vikali na KMC Kuelekea Mechi ya Kesho Mei 11, 2025

Simba Yapewa Vitisho Vikali na KMC Kuelekea Mechi ya Kesho

Simba Yapewa Vitisho Vikali na KMC Kuelekea Mechi ya Kesho Mei 11, 2025

Dar es Salaam – Kikosi cha KMC kimeweka bayana dhamira yake ya kuwapa wakati mgumu Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Jumapili, Mei 11, 2025, kwenye Uwanja wa KMC Complex, wakiahidi ushindani mkali na mshangao mkubwa dhidi ya wapinzani wao hao wa muda mrefu.

Kocha wa muda wa KMC, Adam Mbwana, amefichua kuwa maandalizi ya timu hiyo yamekamilika kwa asilimia kubwa, huku akiweka wazi kuwa mchezo huo wa mwisho kwao kucheza nyumbani msimu huu utakuwa fursa muhimu ya kupambana kwa hali na mali ili kuvuna pointi tatu muhimu. Kwa mujibu wa Mbwana, KMC imefanya mazoezi ya kutosha na kufanya tathmini ya kina kuhusu mechi za Simba zilizopita, hatua ambayo imewapa mwanga kuhusu maeneo ya kuyashambulia kwa ufanisi.

Simba Yapewa Vitisho Vikali na KMC Kuelekea Mechi ya Kesho Mei 11, 2025

“Tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Simba. Huu ni mchezo wa mwisho nyumbani kabla ya kuhitimisha msimu, kwa hiyo ni lazima tuutumie kwa faida yetu kupata ushindi. Tunakwenda kutafuta pointi tatu kwa sababu michezo inayofuata ni mitatu mfululizo ugenini,” alisema Mbwana.

Kocha huyo amesisitiza kuwa Simba ni timu kubwa na yenye ubora, lakini pia ina mapungufu ambayo KMC imepanga kuyatumia kwa makini. Licha ya historia ya Simba dhidi yao, KMC inaamini kwamba ushindi bado ni jambo linalowezekana.

Katika upande wa wapinzani wao, Simba SC, benchi la ufundi linaloongozwa na kocha msaidizi Selemani Matola limeeleza kuwa linafahamu vema hamasa ya KMC kwenye mchezo huo. Matola amethibitisha kuwa kikosi chake kiko tayari kwa pambano hilo, licha ya ratiba ngumu iliyowakabili hivi karibuni.

“Ndani ya siku 10 tumeshacheza mechi tatu, na hii ya KMC ndiyo ya mwisho. Ni mechi ngumu lakini tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunapata alama tatu muhimu,” alisema Matola.

Kwa mujibu wa Matola, Simba itawakosa huduma ya kiungo Mzamiru Yassin pekee kutokana na majeraha, huku wachezaji wengine wote wakiwa fiti kambini. Anaamini kuwa kikosi chake kinao wachezaji wa kutosha wenye uwezo wa kutoa matokeo mazuri licha ya ugumu wa uwanja wa ugenini.

“KMC hawana matokeo mazuri, lakini wana timu nzuri. Ni wapinzani wanaojua kujituma wakiwa nyumbani, hivyo tumejiandaa vilivyo kuhakikisha tunashinda mechi hiyo,” aliongeza.

Kumbukumbu za Mzunguko wa Kwanza na Rekodi ya Simba

Itakumbukwa kuwa katika mzunguko wa kwanza wa msimu huu, Simba waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya KMC katika uwanja huo huo wa KMC Complex, Novemba 6, 2024. Hata hivyo, pamoja na matokeo hayo ya awali, KMC imeapa kutoruhusu historia hiyo ijirudie.

Kwa mujibu wa takwimu, Simba ina rekodi ya kuvutia dhidi ya KMC, ambapo katika mechi 13 zilizowakutanisha, Wekundu wa Msimbazi wameshinda michezo 11 huku miwili ikimalizika kwa sare. KMC bado haijapata ushindi wowote dhidi ya Simba katika Ligi Kuu, hali inayoongeza presha kwa upande wao huku wakiwa na kiu ya kuivunja rekodi hiyo.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Napoli Yajipanga Kumsajili Jack Grealish Kutoka Man City
  2. KENGOLD Yapanga Kuipeleka Simba Ruvuma Juni 18
  3. Simba SC Yakata Tiketi Ligi ya Mabingwa Afrika 2025-2026 Baada ya Kufikisha Pointi 66
  4. Yanga Yashikilia Msimamo wa Kutocheza Dabi Licha Ya Majibu ya CAS
  5. Simba Yaitandika JKT na Kujiweka Kwenye Njia ya Ligi ya Mabingwa
  6. Matokeo JKT Tanzania vs Simba Leo 05/05/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo