Simba vs Berkane Leo 25/05/2025 Saa Ngapi?

Simba vs Berkane Leo Saa Ngapi

Simba vs Berkane Leo 25/05/2025 Saa Ngapi?

Kikosi cha Simba leo kitashuka dimbani katika mtanange wa fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, ambao unatarajiwa kutimua vumbi katika viunga vya Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Ni mechi ya marudiano dhidi ya RS Berkane ya Morocco, ambapo Wekundu wa Msimbazi wanahitaji ushindi wa mabao matatu bila kuruhusu bao ili kutwaa ubingwa wa kihistoria kwa mara ya kwanza.

Tarehe 17 Mei 2025, Simba ilijikuta nyuma kwa mabao 2-0 ndani ya dakika 20 za mwanzo ya mechi ya kwanza iliyochezwa nchini Morocco. Kocha mkuu Fadlu Davids amesema kuwa kipigo hicho kimewapa wachezaji wake uzoefu wa kipekee na ari mpya kuelekea pambano la leo, ambalo ni la mwisho na la kuamua bingwa wa michuano hiyo.

Mechi ya Simba vs Berkane leo 25 Mei 2025 inatarajiwa kuanza saa 16:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Simba vs Berkane Leo 25/05/2025 Saa Ngapi?

Kocha Fadlu ameeleza kuwa Simba ilikuwa imejiandaa vizuri kwa mechi ya awali, lakini changamoto halisi ilitokea katika dakika 20 za mwanzo, jambo alilosema haliwezi kufundishwa darasani bali hutokana na uzoefu wa moja kwa moja. Hata hivyo, alisisitiza kuwa kipindi hicho kifupi kimetoa somo muhimu kwa kikosi chake.

Licha ya kutoshiriki kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Benjamin Mkapa, Kocha huyo anaamini kuwa Zanzibar inaweza kuwa nyumbani kwao kwa msaada wa mashabiki wa Tanzania nzima. “Tunahitaji kuigeuza Zanzibar kuwa nyumbani kwetu. Hilo linawezekana kama Watanzania wataungana na kusimama pamoja nasi,” alisema.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Rais Mwinyi Aahidi Mamilioni Kwa Simba Wakishinda Kombe la Shirikisho
  2. Mamelodi Sundowns Yatoshana Nguvu na Pyramids FC Pretoria
  3. Taifa Stars Kumenyana Kirafiki na Bafana Bafana Afrika Kusini
  4. Yanga Yaagana na Stephane Aziz Ki, Aelekea Wydad AC Morocco
  5. Al-Hilal Yampa Bruno Fernandes Wiki Kujibu Ofa Yao
  6. Timu Zilizopanda Daraja Ligi Kuu Tanzania 2025/2026
  7. Ambokile Aitega Mbeya City Baada Ya Kupanda Daraja
  8. Napoli Yabeba Kombe la Serie A kwa Mara ya Nne Baada Vita Kali Dhidi ya Inter
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo