KIKOSI CHA SIMBA VS BERKANE LEO 25/05/2025 – FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Simba vs Berkane Leo Saa Ngapi

KIKOSI CHA SIMBA VS BERKANE LEO 25/05/2025

Kikosi cha Simba leo kitashuka dimbani katika mtanange wa fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, mchezo wa marudiano dhidi ya RS Berkane ya Morocco, ambao unatarajiwa kutimua vumbi katika viunga vya Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Huu ni mchezo wa kihistoria kwa upande wa klabu ya Simba, ambao wana ndoto ya kutwaa ubingwa wa CAF Confederation Cup kwa mara ya kwanza katika historia yao. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Mei 17, 2025 huko Morocco, Simba ilikubali kichapo cha mabao 2-0 ndani ya dakika 20 za mwanzo, hali iliyowapa kazi ngumu kuelekea mchezo wa leo. Ili kutwaa ubingwa huo, Simba inahitaji ushindi wa mabao matatu bila kuruhusu bao – jambo ambalo linahitaji umakini wa hali ya juu, ari, na mshikamano mkubwa wa timu nzima.

Kocha wa Simba, Fadlu Davids, ameeleza kuwa tukio hilo la kupoteza mabao mapema katika mchezo wa awali limekuwa funzo kubwa kwa wachezaji wake. Amesema hali hiyo imewasaidia wachezaji kuelewa presha ya fainali na umuhimu wa kuwa tayari kimwili na kiakili kuanzia dakika ya kwanza. “Unaweza kuwa na mpango mzuri wa kiufundi, lakini hali halisi ya fainali ni lazima iishiwe na wachezaji wenyewe uwanjani,” alisema Fadlu.

KIKOSI CHA SIMBA VS BERKANE LEO 25/05/2025 – FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Kikosi Cha Simba Vs Berkane Leo 25/05/2025 – Fainali Ya Kombe La Shirikisho

Kikosi rasmi cha Simba kitakachoshuka dimbani leo kinatarajiwa kutangazwa majira ya saa 09:00 alasiri. Tutakuletea orodha kamili ya wachezaji mara tu kocha Faldu Davis atakapokitangaza. Tegemea mchezo wenye ushindani na muto wa kipee, ambapo RS Berkane itakua na jukumu la kuonesha ubabe wake ugenini, huku Simba ikipambana kupindua meza baada ya kushindwa katika mchezo wa kwanza ugenini.

KIKOSI CHA SIMBA VS BERKANE LEO 25/05/2025 – FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Zanzibar Yageuzwa Uwanja wa Nyumbani

Ingawa Simba walitarajia kucheza mchezo wa marudiano katika Uwanja wa Benjamin Mkapa – uwanja wenye historia nzuri kwao – mchezo huu umehamishiwa Zanzibar. Hata hivyo, Kocha Fadlu amesema hawatatumia hilo kama kisingizio. Badala yake, wanatazama fursa ya kugeuza Zanzibar kuwa nyumbani kwa kushirikiana na mashabiki wa soka kutoka kila kona ya Tanzania.

“Tunataka kuigeuza Zanzibar kuwa kama Benjamin Mkapa. Tunaamini Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla watasimama pamoja nasi. Huu ni wakati wa umoja,” alisisitiza.

Fadlu anaamini kuwa sapoti ya mashabiki itakuwa nguvu ya ziada kwa wachezaji wake, huku akiweka bayana kuwa Simba imejifunza kutoka kwa Berkane, na sasa wapo tayari kwa mapambano ya leo.

Matumaini ya Ushindi wa Kihistoria

Katika mchezo wa kwanza, pamoja na kufungwa, Simba ilionesha dalili nzuri hasa katika kipindi cha pili, ambapo walibadilika kimkakati na kufanya mchezo kuwa wa ushindani zaidi. Kocha Fadlu alieleza kuwa pamoja na Berkane kuwa na mabao mawili, takwimu zilionesha kuwa walistahili bao moja tu kwa mujibu wa ‘expected goals’. Mlinzi Mussa Camara alisifiwa kwa kuokoa bao la wazi lililoweza kuongeza maumivu kwa Simba.

Kocha huyo pia alifafanua kuwa alilazimika kuonesha kadi ya njano katika mchezo huo kama njia ya kuwaamsha wachezaji wake na kuwajulisha kuwa walikuwa kwenye vita – jambo lililoamsha ari na dhamira ya wachezaji wake.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Simba vs Berkane Leo 25/05/2025 Saa Ngapi?
  2. Rais Mwinyi Aahidi Mamilioni Kwa Simba Wakishinda Kombe la Shirikisho
  3. Mamelodi Sundowns Yatoshana Nguvu na Pyramids FC Pretoria
  4. Taifa Stars Kumenyana Kirafiki na Bafana Bafana Afrika Kusini
  5. Yanga Yaagana na Stephane Aziz Ki, Aelekea Wydad AC Morocco
  6. Al-Hilal Yampa Bruno Fernandes Wiki Kujibu Ofa Yao
  7. Timu Zilizopanda Daraja Ligi Kuu Tanzania 2025/2026
  8. Ambokile Aitega Mbeya City Baada Ya Kupanda Daraja
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo