Herry Sasii Afungiwa Soka Miezi 6 Kisa Mechi ya Simba na Singida
Mwamuzi Herry Sasii amepigwa marufuku ya miezi sita kujihusisha na mchezo wa soka, baada ya kushindwa kumudu vyema mchezo mkali kati ya Simba SC na Singida Black Stars uliopigwa kwenye dimba la KMC, Dar es Salaam. Kamati ya Usimamizi wa Ligi imechukua hatua hiyo kali baada ya kubaini makosa kadhaa ya kiuamuzi yaliyosababisha dosari kubwa kwenye mechi hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Katika taarifa rasmi ya Kamati hiyo, ilielezwa kuwa Sasii alifanya makosa mengi yaliyodhihirisha udhaifu wa kutafsiri na kutumia ipasavyo sheria 17 za mchezo wa soka. Simba walifanikiwa kushinda mchezo huo kwa bao 1-0, lakini utendaji wa mwamuzi huyo uliibua hisia kali kutoka kwa wadau wa soka na mashabiki, hali iliyosababisha uchunguzi wa kina kufanyika dhidi yake.
Adhabu Zilizotolewa Kwa Wadau Wengine
Mbali na Herry Sasii, baadhi ya watu wengine pia wamewajibishwa kufuatia vurugu na matukio yasiyofaa yaliyojitokeza wakati na baada ya mchezo huo.
Fadlu Davids – Kocha Mkuu wa Simba: Kocha wa Simba SC, Fadlu Davids, ametozwa faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000 TZS) kwa kosa la kutoa matamshi dhidi ya Bodi ya Ligi. Kauli hizo zilitafsiriwa kama ni shambulio la moja kwa moja kwa uongozi wa ligi, hivyo Kamati ikaona ni vyema kuchukua hatua ya kinidhamu dhidi yake.
Reidoh Berdien – Kocha Msaidizi Simba: Kocha msaidizi wa Simba, Reidoh Berdien, naye hakuepuka mkono wa sheria. Amepigwa marufuku ya mechi tatu pamoja na kutozwa faini ya shilingi milioni moja (1,000,000 TZS) kwa kosa la kuanzisha vurugu kwa kurusha koni kuelekea benchi la timu ya Singida. Kitendo hicho kilionekana kuchochea taharuki isiyofaa uwanjani.
Jonathan Sowah – Mshambuliaji wa Singida Black Stars: Mchezaji wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah, naye ameadhibiwa kwa kitendo cha utovu wa nidhamu baada ya kuwaonyesha mashabiki wa Simba ishara ya matusi na kung’oa kibendera uwanjani. Kamati imemtoza faini ya shilingi milioni moja (1,000,000 TZS) kama adhabu kwa tabia hiyo isiyokubalika katika mchezo wa kiungwana.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Seif Karihe Acharazwa Faini na Kufungiwa Michezo Mitatu kwa Kurusha Chupa
- Ronaldo Aipeleka Ureno Fainali UEFA Nations League 2024/2025
- Matokeo ya Germany Vs Portugal Leo 04/06/2025
- Wachezaji wa Soka U-21 Waliofanya Vizuri Msimu wa 2024/2025
- Mabekio Waliochangia Magoli Mengi Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
- Siku ya Kuripoti Chuo cha Polisi Moshi 2025 kwa Vijana Waliochaguliwa
- Michezo ya Yanga Sc Iliobaki Msimu wa 2024/2025
Leave a Reply