Matokeo ya Mashujaa Vs Dodoma Jiji Leo 17/08/2024
Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea kushika kasi, na leo mashabiki wa soka Tanzania watashuhudia mtanange mkali kati ya Mashujaa FC na Dodoma Jiji FC. Mechi hii inatarajiwa kuwa ya kusisimua, hasa kwa kuzingatia historia ya michezo kati ya timu hizi mbili.
Taarifa kuhusu Mechi
- 🏆 #NBC Tanzania Premier League
- Mashujaa Fc🆚Dodoma Jiji
- 📆 17.08.2024
- 🏟 Uwanja wa Tanganyika kigoma
- 🕖 Saa Kumi Kamili
Fuatilia Hapa Matokeo ya Mashujaa Vs Dodoma Jiji Leo
Mashujaa FC | 1-0 | Dodoma Jiji |
Takwimu za Mechi Zilizopita: Mashujaa FC dhidi ya Dodoma Jiji FC
Timu hizi zimekutana mara kadhaa katika mechi za hivi karibuni na matokeo yanaonyesha ushindani mkubwa. Katika mechi ya mwisho iliyofanyika tarehe 28 Mei 2024, Mashujaa FC iliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC. Hata hivyo, katika mchezo wa tarehe 11 Februari 2024, timu hizi zilitoka sare ya bao 1-1.
Matokeo ya Timu Katika Mechi Zilizopita
Takwimu zinaonyesha kuwa Mashujaa FC imekuwa na mwenendo mzuri katika mechi zake za hivi karibuni. Katika mechi tano za mwisho, Mashujaa FC imeshinda mechi nne na kupoteza moja tu, huku ikifunga mabao 11 na kuruhusu mabao 4 tu.
Kwa upande mwingine, Dodoma Jiji FC imekuwa na wakati mgumu, kwani katika mechi zao tano za mwisho, wameshinda mechi moja tu, wameruhusu mabao 8 na kufunga mabao 2 pekee.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti