PSG Yatinga Nusu Fainali Baada ya Kuichapa Bayern Munich 2-0 Marekani
Paris Saint-Germain (PSG) imeandika historia baada ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya vigogo wa Ujerumani, Bayern Munich, katika mchezo mkali wa robo fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu nchini Marekani. Mtanange huu uliojaa drama na kusisimua ulipigwa katika dimba la Mercedes-Benz, Atlanta, Georgia, na kuishuhudia PSG ikitinga nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa.
Mabingwa hao wa Ufaransa, licha ya kumaliza mchezo wakiwa pungufu ya wachezaji wawili kutokana na kadi nyekundu, walionyesha uthabiti na ubora wa hali ya juu dhidi ya Bayern, waliokuwa wameshinda mechi zao nne zilizopita dhidi ya PSG, ikiwemo ushindi wa 1-0 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi Novemba mwaka jana.
Muhtasari wa Mchezo: Drama Hadi Dakika ya Mwisho
Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikicheza soka la kushambulia na la pasi fupi fupi, zikionyesha uwezo mkubwa wa kukaba na kupiga pasi. Hali ya hewa iliyo nogeshwa na viyoyozi katika uwanja wa Mercedes-Benz ilichangia kuwepo kwa mchezo wa kusisimua, uliowashirikisha wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu wa kukokota mpira na makipa wawili bora duniani, Gianluigi Donnarumma wa PSG na Manuel Neuer wa Bayern.
Nafasi za kufunga zilianza kuonekana mapema kwa pande zote. Desire Doue alipiga shuti kidogo nje ya lango la Bayern, huku Donnarumma akipangua shuti la Michael Olise. Khvicha Kvaratskhelia naye alikaribia kufunga baada ya shambulizi kali la PSG, kabla ya Donnarumma kufanya kazi ya ziada kupangua tena shuti la Olise.
Manuel Neuer pia alifanya kazi kubwa kuokoa shuti kali la Kvaratskhelia, lililopigwa baada ya mpira mrefu kutoka kwa Bradley Barcola. Donnarumma kwa upande wake aliokoa krosi ya Aleksandar Pavlovic iliyomkosa Musiala na karibu kuingia wavuni.
Bao la Dayot Upamecano kwa Bayern lilikataliwa kutokana na kuotea. Nahodha wa Uingereza, Harry Kane naye alikaribia kufunga kwa kichwa baada ya kazi nzuri ya Kingsley Coman.
Majeraha na Kadi Nyekundu Zatawala
Mchezo ulikumbwa na pigo kubwa kabla ya mapumziko baada ya kiungo mahiri wa Bayern, Jamal Musiala, kupata jeraha baya la kifundo cha mguu kufuatia kugongana na Donnarumma, tukio lililomwacha kipa huyo wa Italia akiwa amechanganyikiwa.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ile ile, huku Neuer akifanya kazi ya ajabu kuokoa shuti la Barcola aliyeingia ndani ya eneo la hatari. Kocha wa PSG, Luis Enrique, aliamua kumwingiza Ousmane Dembele dakika 20 za mwisho ili kutafuta tofauti na kuepuka muda wa nyongeza, ambao haukuhitajika baada ya msimu mrefu na mgumu.
Dembele alikaribia kufunga baada ya Neuer kutoa mpira vibaya nje ya eneo lake, lakini shuti lake lilipita sentimita chache nje ya lango tupu. Hatimaye, kinda Desire Doue mwenye umri wa miaka 20 aliipa PSG bao la kwanza, akitumia makosa ya Kane na kufunga kwa shuti la chini kwenye lango la karibu.
Hofu iliingia kwa PSG baada ya beki wao Willian Pacho kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 83 kwa kumchezea vibaya Leon Goretzka. Kane alifunga bao lililokataliwa kwa kuotea kabla ya Lucas Hernandez wa PSG naye kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na kumpiga kiwiko mpinzani. Licha ya kuwa pungufu ya wachezaji wawili, PSG walishikilia ushindi wao na Dembele alihitimisha ushindi kwa kufunga bao la pili baada ya Achraf Hakimi kupiga pasi nzuri.
Heshima kwa Diogo Jota na Maandalizi ya Nusu Fainali
Kabla ya mchezo kuanza, wachezaji na mashabiki wapatao 67,000 walishika kimya cha dakika moja kwa heshima ya mshambuliaji wa Liverpool, Diogo Jota, na kaka yake Andre Silva, waliofariki kwa ajali ya gari Alhamisi iliyopita. Ilikuwa ni wakati wa hisia kali, hasa kwa upande wa PSG wenye wachezaji watano kutoka Ureno, ikiwemo wachezaji muhimu kama Vitinha, Joao Neves na Nuno Mendes. Baada ya kufunga bao la pili, Dembele alisherehekea kwa “style” ya Diogo Jota, akimuenzi Mreno huyo aliyefariki.
Kwa ushindi huu, PSG sasa wanasubiri mshindi kati ya Real Madrid na Borussia Dortmund, ambao watachuana katika nusu fainali nyingine itakayopigwa Jumatano ijayo katika uwanja wa MetLife, New Jersey. Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali na wa kuvutia, huku PSG wakitarajiwa kuendeleza kasi yao ya ushindi katika michuano hii mikubwa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Namungo Yampigia Hesabu Ally Salim Kama Mrithi wa Beno Kakolanya
- Tetesi Za Usajili Simba Leo 2025/2026
- Wallace Karia Abaki Bila Mpinzani Baada ya Wagombea Watano Kuenguliwa
- Ibenge Atua Tanzania Kujiunga Rasmi na Azam FC kwa Msimu wa 2025/26
- Tetesi Za Usajili Yanga Leo 2025/2026
- Makombe ya Yanga 2024/2025
- Florent Ibenge Aaga Rasmi Al Hilal Sudan, Aelekea Kujiunga na Azam FC
- Lionel Messi anukia Ligi Kuu ya Uingereza EPL
- Miloud Hamdi Ajiunga na Ismaily ya Misri Baada ya Kuipa Yanga Mataji 3
Leave a Reply