Matokeo KMC vs Coastal Union Leo 29/08/2024 | Matokeo ya Mechi ya KMC leo dhidi Coastal Union
Leo tarehe 29 Agosti 2024, mashabiki wa soka watashuhudia pambano kali kati ya KMC na Coastal Union katika Uwanja wa KMC, Mwenge, Dar es Salaam. Mchezo huu unatarajiwa kuanza majira ya saa 10 jioni na umevutia hisia nyingi kutokana na rekodi za timu hizi mbili zinapokutana.
KMC na Coastal Union zimekutana mara 12 tangu msimu wa 2018/19 ambapo KMC ilipoanza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara. Katika mikutano hii, sare zimekuwa nyingi, zikitokea mara saba. Coastal Union wamefanikiwa kushinda michezo mitatu huku KMC ikipata ushindi mara mbili, mmoja wapo ukiwa ni ushindi mkubwa wa mabao 5-2 msimu wa kwanza wa KMC.
Mara ya mwisho timu hizi zilikutana msimu uliopita, na matokeo yalikuwa sare katika michezo yote miwili nyumbani na ugenini. Hii inaonyesha jinsi ambavyo timu hizi zinavyolingana katika uwezo na ushindani, jambo linalowafanya mashabiki kutarajia pambano lenye mvutano mkubwa leo.
Kocha wa KMC, Abdi Hamid Moallin, ameeleza kuwa timu yake imejiandaa vyema kwa ajili ya mechi hii, akisisitiza umuhimu wa kutumia faida ya kucheza nyumbani. Moallin alisema, “Ni mchezo wetu wa kwanza wa ligi, naamini utakuwa mgumu lakini wachezaji wapo tayari tukifahamu kwamba ligi ni ngumu. Tutatumia faida ya uwanja wetu wa nyumbani kusaka matokeo mazuri.”
Kwa upande wa Coastal Union, kocha wao Ngawina Ngawina ameonyesha heshima kwa wapinzani wao akisema kuwa wanatambua ubora wa KMC. Ngawina alisema, “Msimu uliopita KMC walimaliza ligi nyuma yetu kwa nafasi moja, tunawaheshimu wana mwalimu mzuri na kikosi kizuri. Tumejipanga kukabiliana nao kwani tunawafahamu vizuri.”
Matokeo KMC vs Coastal Union Leo 29/08/2024
KMC FC | 1-0 | Coastal Union Fc |
- 🏆 #NBCPremierLeague@ Matokeo KMC vs Coastal Union Leo
- ⚽️ KMC FC🆚Coastal Union Fc
- 📆 29.08.2024
- 🏟 Kaitaba
- 🕖 10:00 Jioni
Tathmini ya Mchezo na Matarajio
Kutokana na historia na maandalizi ya timu zote mbili, mechi hii inatarajiwa kuwa na ushindani mkali. Coastal Union wakiwa na kumbukumbu ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na AS Bravos ya Angola kwa mabao 3-0, wanahitaji ushindi ili kuanza msimu kwa mafanikio. Kwa upande wa KMC, kucheza nyumbani kunawapa motisha ya kufanya vizuri na kuanza ligi kwa alama tatu.
Timu zote mbili zinaingia kwenye mchezo huu zikiwa na lengo la kuanza msimu kwa ushindi, na hii inatarajiwa kuongeza hamasa na mbinu za kimchezo katika dakika zote 90 za mchezo.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Viingilio Mechi ya Kirafiki Simba Vs Al Hilal 31/08/2024
- Viingilio Mechi ya Kagera Sugar Vs Yanga Leo 29/08/2024
- Matokeo Kagera Sugar Vs Yanga Leo 29/08/2024
- Kikosi cha Yanga Vs Kagera Sugar Leo 29/08/2024
- RATIBA ya Mechi za Leo 29 August 2024
- Nyota Wawili Yanga Kuikosa Kagera Sugar
- Mabadiliko ya Ratiba Mechi ya Kagera Sugar vs Yanga
Weka Komenti