Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 (NECTA Form Six Results)
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza rasmi Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 (NECTA Form Six Results), baada ya kukamilika kwa mtihani huo uliofanyika kuanzia Mei 5 hadi 26, 2025.
Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu, Julai 7, 2025 visiwani Zanzibar na Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohamed, akibainisha viwango vya ufaulu, hali ya udanganyifu, na hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika.
Kwa mujibu wa Prof. Said, wanafunzi 125,779, ambao ni asilimia 99.95% ya watahiniwa wa shule, wamefaulu mtihani wa kidato cha sita mwaka huu, ikilinganishwa na asilimia 99.92% mwaka 2024. Hii inaonesha ongezeko la ufaulu kwa 0.03%, jambo linalotafsiriwa kuwa ni dalili chanya ya kuboreka kwa mfumo wa elimu nchini.
NECTA Yafuta Matokeo kwa Sababu za Udanganyifu
Pamoja na mafanikio hayo, Baraza la Mitihani la Tanzania limetangaza kufuta matokeo ya watahiniwa 71 waliobainika kufanya udanganyifu. Kati yao, 70 walikuwa wa kidato cha sita (ikiwa ni 64 kutoka shule za kawaida na 6 wa kujitegemea) na mwanafunzi mmoja wa mtihani wa Ualimu Daraja A (GATCE). Hatua hiyo imetolewa chini ya mamlaka ya Kifungu cha 5(2)(i) na (j) cha Sheria ya Baraza la Mitihani Sura ya 107, pamoja na Kifungu cha 30(2)(b) cha Kanuni za Mitihani za mwaka 2016.
Lengo Kuu la Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE)
Mtihani wa ACSEE (Advanced Certificate of Secondary Education Examination) una malengo mahususi katika maendeleo ya elimu ya juu kwa wanafunzi:
- Kupima uwezo wa mwanafunzi kujiunga na elimu ya juu kama vyuo vikuu na taasisi za elimu ya kati.
- Kutathmini ujuzi na maarifa ya mwanafunzi, ikiwa ni maandalizi ya maisha ya baadaye kazini au kitaaluma.
- Kuthibitisha kiwango cha uelewa wa mwanafunzi katika masomo mbalimbali kama PCM, EGM, HGL, ECA, nk.
Wanafunzi waliohitimu wanatarajiwa kuonesha uelewa wa kina wa kimaudhui, kuchambua hoja, kuunganisha dhana, na kutoa tathmini sahihi kwa misingi ya kitaaluma.
Je, Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 Yalitangazwa Lini?
Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 (NECTA Form Six Results) yametangazwa rasmi Julai 7, 2025, ambayo ni mapema ukilinganisha na baadhi ya miaka iliyopita. Tazama mwenendo wa miaka iliyotangulia:
Mwaka | Tarehe ya Matokeo |
2025 | Julai 07 |
2024 | Julai 13 |
2023 | Julai 13 |
2022 | Julai 5 |
2021 | Julai 10 |
2020 | Agosti 21 |
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 (NECTA Form Six Results)
NECTA imeanzisha njia mbalimbali za kuwasaidia wanafunzi na wazazi kupata Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 kwa urahisi:
1. Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 Kupitia Mtandao (Online)
Hapa tumekurahisishia zoezi la kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 (NECTA Form Six Results) kwa kukuletea viungo vya moja kwa moja vitakavyokuwezesha kuona matokeo ya shule yako moja kwa moja. Ili kuangalia matokeo ya shule yako:
🔍 Tafuta jina la shule kwenye orodha hapa chini kisha bonyeza jina hilo ili kufungua matokeo moja kwa moja.
ALL CENTRES | A | B | C | D | E | F |
G | H | I | J | K | L | |
M | N | O | P | Q | R | S |
T | U | V | W | X | Y | Z |
Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 (NECTA Form Six Results 2025)
Kumbuka: Viungo vya majina ya shule vitakupeleka moja kwa moja kwenye ukurasa wa NECTA wa matokeo ya Kidato cha Sita kwa shule husika. Kama jina la shule yako halipo kwenye orodha hii fupi, bonyeza herufi ya mwanzo ya jina la shule yako kwenye orodha ya ALL CENTRES ili kuipata.
2. Kuangalia Matokeo ya Kidato cha Sita Kupitia USSD – Simu ya Mkononi (Bila Intaneti)
Njia hii ni nzuri kwa walio kwenye maeneo yenye changamoto ya mtandao:
- Piga *152*00# kwenye simu yako.
- Chagua namba 8 – Elimu, kisha namba 2 – NECTA.
- Chagua namba 1 – Matokeo, halafu namba 2 – ACSEE.
- Ingiza namba ya mtihani (mfano: S0334/0556/2025).
- Chagua njia ya malipo (gharama ya kawaida ni Tsh 100/=).
- Utapokea matokeo yako kwa SMS.
3. Kupitia Shule Husika
Shule nyingi hupokea nakala rasmi ya matokeo kutoka NECTA na kuyabandika kwenye ubao wa matangazo. Wanafunzi wanaweza kwenda shuleni au kuwasiliana na walimu ili kusaidiwa kuona matokeo yao.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Tarehe ya Kutangazwa kwa Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 na NECTA
- Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 NECTA ACSEE
- Fomu Za Kujiunga Kidato Cha Tano (Form Five Joining Instruction Form) 2025
- Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano 2025/2026 (Form Five Selection)
- Shule Walizopangiwa Kidato cha Tano Zanzibar 2025
- Majina ya Waliochaguliwa Vyuo Vya Kati 2025/2026 (Selection Vyuo Vya Kati)
- Waliochaguliwa Kidato Cha Tano na Vyuo vya Kati 2025 (Tamisemi Selection)
Leave a Reply