Viingilio Mechi ya Yanga Vs CBE 21/09/2024 | Bei ya Tikeki za Kutazama Mechi ya Yanga Vs CBE SA
Mabingwa watetezi wa Tanzania, Yanga SC, wanajiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya CBE SA ya Ethiopia, itakayofanyika kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar tarehe 21 Septemba 2024.
Mchezo huu ni sehemu ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika 2024/2025, na ni wazi kuwa utavutia mashabiki wengi kutokana na ushindani wa timu zote mbili. Katika mchezo wa awali, Yanga SC walishinda kwa goli 1-0, lakini CBE SA wameonesha uwezo wa kurekebisha makosa yao, jambo linalofanya mechi hii ya marudiano kuwa ya kusisimua zaidi.
Kama unataka kushuhudia mchezo huu live uwanjani, unahitaji kujua bei ya tiketi za viingilio na wapi unaweza kukata tiketi zako mapema ili kuepuka usumbufu wa dakika za mwisho. Hapa, tumekuletea orodha ya vituo rasmi vinavyo toa huduma ya kuuza tiketi za kutazama mchezo huu, bei za viingilio, na kila kitu unachopaswa kujua kabla ya mechi kubwa kati ya Yanga SC na CBE SA.
Viingilio Mechi ya Yanga Vs CBE 21/09/2024
Kwa mashabiki wanaotaka kushuhudia mechi hii ya kusisimua, bei za viingilio zimetangazwa ili kila mtu aweze kupanga bajeti yake ipasavyo. Hapa chini ni viwango vya tiketi kulingana na maeneo tofauti uwanjani:
- SAA – Tsh 5,000
- ORBIT – Tsh 10,000
- URUSI – Tsh 15,000
- WINGS – Tsh 20,000
- VIP – Tsh 30,000
Vituo Vya Kukata Tiketi
Ili kuhakikisha kwamba mashabiki wote wanapata fursa ya kukata tiketi zao kwa urahisi, Yanga SC imeweka vituo kadhaa vya kuuza tiketi. Hapa ni orodha ya vituo vilivyoidhinishwa ambapo unaweza kukata tiketi zako:
- Young Africans – Jangwani
- Uwanja Wa Amaan, Znz (Amaan Stadium, Zanzibar)
- Zff – Zanzibar
- Ttcl – Kijangwani, Znz
- Vunja Bei – Michenzani Mall
- Uwanja Wa Amaan Kwa Harith
- Mwinyi Mwanakwerekwe – Car Wash
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti