Tetesi za Usajili Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2025/2026
Baada ya msimu wa 2024/2025 kumalizika kwa shamrashamra za mafanikio kwa baadhi ya vilabu, sasa ni muda wa timu mbalimbali kujipanga upya kwa ajili ya msimu ujao wa 2025/2026. Msimu huu mpya unatarajiwa kuwa na ushindani mkali zaidi, hasa ikizingatiwa kuwa Yanga SC ilimaliza msimu uliopita kwa kuzoa mataji yote ya ndani – jambo linaloweka presha kwa wapinzani wao kuimarisha vikosi.
Dirisha la Usajili Lafunguliwa Rasmi
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilitangaza rasmi kuwa dirisha kubwa la usajili kwa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Championship, First League, Ligi Kuu ya Vijana (U-20), pamoja na Ligi ya Wanawake limefunguliwa kuanzia Julai 1, 2025 na linatarajiwa kufungwa mnamo Septemba 7, 2025 saa 5:59 usiku.
Kwa mujibu wa TFF, usajili wa wachezaji unafanyika kupitia mfumo rasmi wa FIFA Connect, na klabu zimetakiwa kuwasilisha nyaraka kamili na sahihi ili kuidhinishwa kwa wakati. TFF pia imesisitiza kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe ya mwisho kupita.
Simba SC Yaanza Msimu kwa Sajili Nzito
Klabu ya Simba imefungua ukurasa mpya wa usajili kwa kumpata kiungo wa ulinzi Balla Moussa Conte, raia wa Guinea mwenye umri wa miaka 21 kutoka CS Sfaxien ya Tunisia. Conte alikuwa na mkataba unaomalizika 2026, lakini Simba imevunja mkataba huo na kumsajili kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba.
Msimu uliopita, Conte alicheza jumla ya mechi 34, zikiwemo 23 za Ligi Kuu ya Tunisia, 6 za Kombe la Shirikisho Afrika, na 2 za Kombe la Klabu Bingwa kwa Nchi za Kiarabu, huku akionyeshwa kadi 7 za njano. Usajili wake unakuja baada ya Simba kuachana na viungo wake wawili, Fabrice Ngoma na Augustine Okejepha, hivyo kuweka nafasi wazi kwa chipukizi huyo.
Aidha, Simba imefanya uamuzi wa kumrudisha kwa mkopo kiungo wake mshambuliaji Omary Omary katika klabu ya zamani ya Mashujaa FC, kufuatia kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza.
Azam FC Yatikisa Dirisha la Usajili
Azam FC imejipanga kwa msimu mpya chini ya Florent Ibenge, ambaye ni kocha mpya rasmi:
Wamesajili nyota kadhaa, akiwemo Aishi Manula (kutoka Simba), Lameck Lawi (Coastal Union), na Muhsin Malima (ZED FC, Misri).
- Clatous Chama, ambaye mkataba wake na Yanga umeisha, anawindwa vikali na Azam huku pia akihusishwa na Zesco United.
- Manishimwe Djabel amesaini Azam FC.
- Himid Mao Mkami anatarajiwa kurejea Azam FC.
- Basiala Agey na Ahmed Bakari Pipino wanawindwa na klabu hiyo.
- Kama mambo hayatabadilika, Lameck Lawi ataelekea Azam rasmi.
Mbali na hao, Azam FC pia iko katika mazungumzo na kiungo wa zamani wa Yanga SC, Clatous Chama, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja. Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, kocha Florent Ibenge anamuona Chama kama mchezaji muhimu wa kuziba pengo la Feisal Salum ‘Fei Toto’, ambaye hatima yake ndani ya klabu bado haijafahamika.
Hata hivyo, Azam inakabiliwa na ushindani kutoka klabu ya zamani ya Chama, Zesco United ya Zambia, ambayo pia inamtaka mchezaji huyo kurejea kikosini.
Chama aliyejiunga na Yanga mnamo Julai 1, 2024, alihusika kwenye mabao 9 msimu uliopita — akifunga 6 na kutoa 3 assists — na alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda makombe matano ikiwemo Ligi Kuu ya NBC, Kombe la FA, Ngao ya Jamii, Kombe la Muungano, na Kombe la Toyota.
Namungo FC Yasajili Wachezaji Chipukizi
Namungo FC haikubaki nyuma katika dirisha hili, baada ya kuwasajili wachezaji wawili kutoka Ligi ya Championship:
- Cyprian Kipenye – kutoka Songea United
- Abdulaziz Shahame – kutoka TMA FC ya Arusha
Wachezaji hawa walionyesha kiwango bora katika msimu wa 2024/2025 na sasa wanapewa nafasi ya kuthibitisha uwezo wao katika Ligi Kuu.
Singida Black Stars Wafyekelea Wachezaji
Singida Black Stars imeanza mchakato wa kusafisha kikosi chake kwa ajili ya msimu wa 2025/2026 kwa kuvunja mikataba ya viungo wawili wa kimataifa:
- Emmanuel Bola Labota – raia wa DR Congo
- Matthew Odongo – raia wa Uganda
Wachezaji hao walionekana kutopata nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza, hali iliyosababisha klabu kuchukua hatua ya kuwaachia ili kupisha usajili mpya.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Kikosi cha Taifa Stars Kinaendelea Kujifua Nchini Misri kwa Ajili ya CHAN 2025
- Kocha wa Yanga Miloud Hamdi Ashinda Tuzo ya Kocha Bora wa NBC June 2024
- Simba Yathibitisha Kumtoa Omary Omary kwa Mkopo kwenda Mashujaa FC
- Pacome Zouzoua Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Ligi Kuu Tanzania Bara Juni
- Kibabage Akaribia Kujiunga Singida Bs Baada ya Kumaliza Mkataba Yanga
- Simba Yamalizana na Kiungo Balla Moussa Conte Kutokea CS Sfaxien
- Kocha Mpya wa Yanga 2025/2026: Siri Yafichuka Jangwani!
- Wachezaji 6 wa KMC Wasubiri Hatima Yao Kufuatia Mikataba Kumalizika
- Kennedy Musonda Atimkia Israel Baada ya Kumaliza Mkataba na Yanga
Leave a Reply