Thamani ya Kombe La Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) | Pesa Zinazotolewa Kombe La Shirikisho Afrika 2024/2025 | Kiasi cha Pesa Kinachotolewa CAF Confederation Cup | Zawadi za Kombe La Shirikisho Afrika CAF
Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup), ni mashindano ya pili kwa ukubwa baada ya klabu bingwa Afrika (CAF Champions league) kwa vilabu vya soka barani Afrika. Mashindano haya yamepitia mabadiliko makubwa ambayo yataongeza thamani na mvuto wake. Mabadiliko haya, yaliyotangazwa na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, yana lengo la kuimarisha mashindano ya vilabu na kutoa msaada zaidi wa kifedha kwa vilabu vitakavyo shiriki michuano hii.
Moja ya mabadiliko makubwa yaliyofanywa ni ongezeko kubwa la zawadi za fedha kwa washindi na washiriki wa michuano ya kombe la Shirikisho Afrika. Mshindi wa Kombe la Shirikisho sasa atajinyakulia kitita cha dola za Kimarekani milioni 2, ongezeko kubwa kutoka dola milioni 1.2 za mwaka 2022. Hii ni hatua kubwa katika kuongeza thamani ya mashindano na kuvutia vilabu zaidi kushiriki.
Thamani ya Kombe La Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup)
Hatua | Zawadi |
Mshindi | Dola za Kimarekani 2,000,000 |
Mshindi wa pili | Dola za Kimarekani 1,000,000 |
Nusu fainali | Dola za Kimarekani 750,000 |
Robo fainali | Dola za Kimarekani 550,000 |
Nafasi ya 3 Katika Kundi | Dola za Kimarekani 400,000 |
Nafasi ya 4 Katika Kundi | Dola za Kimarekani 400,000 |
Zawadi kwa Timu Zinazoshiriki Hatua za Mwanzoni (Preliminary Round)
Kwa mara ya kwanza katika historia, CAF itatoa msaada wa kifedha kwa vilabu vinavyoshiriki katika hatua za awali za mashindano.
Kila klabu itakayo shiriki katika raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho itapokea dola 50,000. Hii itasaidia kupunguza gharama za usafiri na vifaa kwa vilabu, na kuwezesha vilabu zaidi, ikiwemo vile vyenye rasilimali chache, kushiriki katika mashindano ya kimataifa.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Manchester United Yaichapa Fulham Katika Mchezo Wa Ufunguzi wa EPL
- Kikosi Cha Yanga VS Vitalo Leo 17/08/2024 CAF
- Matokeo ya Vitalo Vs Yanga Leo 17/08/2024 CAF
- Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)
- Ahmed Arajiga Ateuliwa na CAF Kuchezesha Mechi ya Klabu Bingwa Afrika
- Yanga SC Yaibua Matumaini ya Kufika Nusu Fainali CAF
Weka Komenti