Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Uhasibu TIA 2025/2026

Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Uhasibu TIA 2025/2026

Chuo cha TIA (Tanzania Institute of Accountancy), almaarufu kama Chuo cha Uhasibu, ni miongoni mwa taasisi za elimu ya juu zilizojiwekea heshima kubwa nchini Tanzania kwa kutoa mafunzo bora ya biashara, uhasibu na usimamizi wa rasilimali. Kilianzishwa rasmi kama Shirika la Umma chini ya Wizara ya Fedha kwa mujibu wa Amri ya Serikali Na. 489 ya mwaka 2002, na kinaendesha shughuli zake kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika ya Umma Sura ya 245 (toleo la mwaka 2002). Tangu kuanzishwa kwake, TIA imeendelea kupanuka kwa kasi, ikihudumia wanafunzi kupitia kampasi zake saba zilizopo Dar es Salaam, Mbeya, Singida, Mwanza, Mtwara, Kigoma na Zanzibar.

Kwa mwaka wa masomo 2025/2026, wanafunzi watakaotaka kujiunga na TIA wanapaswa kuzingatia sifa maalum kulingana na ngazi wanayokusudia kujiunga nayo. Ifuatayo ni mwongozo rasmi wa sifa za kujiunga na Chuo cha Uhasibu TIA 2025/2026:

Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Uhasibu TIA 2025/2026

Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Uhasibu TIA Ngazi ya Cheti cha Awali (Basic Technician Certificate)

Mwombaji wa ngazi hii anatakiwa awe na moja ya sifa zifuatazo:

  • Awe amefaulu angalau masomo manne (4) kwa kiwango cha alama “D” au zaidi katika mtihani wa kidato cha nne; au
  • Awe amehitimu ngazi ya NVA II, pamoja na ufaulu wa angalau masomo mawili katika mtihani wa kidato cha nne.

Ngazi hii ni mwanzo mzuri kwa wale waliomaliza kidato cha nne na wanataka kuanza safari ya kitaaluma katika nyanja za uhasibu, ununuzi, au usimamizi wa biashara.

Sifa za Kujiunga na Chuo Cha Uhasibu TIA 2025/2026 Ngazi ya Stashahada (Ordinary Diploma)

Kwa wanaotaka kujiunga na programu ya stashahada, wanapaswa kuwa na mojawapo ya sifa hizi:

  • Awe amehitimu Cheti cha Awali (NTA Level 4) na pia awe na ufaulu wa masomo angalau manne (4) katika mtihani wa kidato cha nne; au
  • Awe amehitimu kidato cha sita, akiwa na Principal Pass moja na Subsidiary moja; au
  • Awe amehitimu NVA III, pamoja na ufaulu wa masomo mawili katika mtihani wa kidato cha nne.

Hii ni hatua ya kati kwa wanafunzi waliokwishaanza elimu ya juu au waliomaliza kidato cha sita na kutamani taaluma ya uhasibu na biashara.

Sifa za Kujiunga na Shahada (Bachelor Degree)

Kwa wale wanaotaka kujiunga na shahada ya kwanza katika moja ya kozi za TIA, sifa ni kama zifuatazo:

I. Wahitimu wa Kidato cha Sita:

Wanaohitimu wanapaswa kuwa na Principal Pass mbili (2) au zaidi, isipokuwa masomo ya dini. Jumla ya alama (points) lazima zifikie 4.0 au zaidi, kulingana na viwango vifuatavyo:

  • Kwa waliohitimu mwaka 2014 na 2015: A = 5, B+ = 4, B = 3, C = 2, D = 1
  • Kwa waliohitimu kabla ya 2014 au baada ya 2015: A = 5, B = 4, C = 3, D = 2, E = 1

Kwa kozi za Uhasibu (BAC), Ununuzi na Ugavi (BPLM), na Uhasibu wa Fedha za Umma (BPSAF), mwombaji lazima awe amefaulu Hisabati na Kiingereza katika kidato cha nne.

II. Wenye Stashahada:

Awe amehitimu Stashahada ya NTA Level 6 kwa GPA ya 3.5 au upper second class; au

Awe amehitimu FTC kwa wastani wa alama ya “B”; au

Awe amehitimu Stashahada ya Ualimu kwa wastani wa alama ya “B+”.

Sifa za Kujiunga na Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma)

Wanaotaka kusoma stashahada ya uzamili katika TIA, lazima wawe na mojawapo ya sifa zifuatazo:

  • Awe na shahada ya kwanza au stashahada ya juu kutoka chuo kinachotambuliwa na NACTVET au TCU; au
  • Awe amepitia ngazi ya kati (intermediate stage) au zaidi katika bodi za taaluma kama NBAA au PSPTB, yaani:
  • NBAA: Ngazi ya Intermediate au zaidi.
  • PSPTB: Ngazi ya Professional Level 3 au zaidi.

Jinsi ya Kutuma Maombi ya Kujiunga Chuo Cha Uhasibu TIA 2025/2026

Kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026, Chuo cha Uhasibu TIA kimeweka mfumo rafiki ambao unawawezesha wanafunzi kutuma maombi ya kujiunga na chuo hiki kwa njia ya mtandao (online application) ili kurahisisha upokeaji wa wanafunzi wapya kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania. Ili kuhakikisha unajisajili kwa usahihi na kwa wakati, fuata hatua hizi muhimu:

Hatua kwa Hatua za Kutuma Maombi:

Hatua kwa Hatua za Kutuma Maombi:

  1. Tembelea Tovuti Rasmi ya TIA
    Fungua www.tia.ac.tz na bofya sehemu ya “Apply Online” au nenda moja kwa moja kwenye mfumo wa maombi kupitia:
    👉 https://oas.tia.ac.tz/login

  2. Unda Akaunti Mpya (Create Account)

    • Bonyeza “Create Account” kwenye ukurasa wa kuingia (login).

    • Jaza namba ya mtihani wa kidato cha nne (Form Four) (sitting ya kwanza) pamoja na mwaka wa kuhitimu kisha bonyeza “Submit”.

    • Thibitisha jina lako, mwaka wa kuhitimu na namba ya mtihani.

    • Chagua ngazi unayoomba: Cheti, Diploma, Shahada, au Stashahada ya Uzamili.

    • Weka barua pepe, chagua na thibitisha nywila (password), na ongeza namba ya simu yako.

    • Bonyeza “Finish” ili kukamilisha usajili, kisha ingia (Login) kutumia taarifa ulizoweka.

  3. Jaza Taarifa Binafsi

    • Baada ya kuingia, jaza taarifa kama: tarehe ya kuzaliwa, jinsia, wilaya, mkoa, na taarifa za mlezi au ndugu wa karibu.

  4. Wasilisha Taarifa za Elimu

    • Ingiza matokeo yako ya kitaaluma kulingana na ngazi unayoomba (kwa mfano: kidato cha nne/sita, cheti, diploma n.k.).

    • Ikiwa inahitajika, pakia vyeti husika (softcopies).

  5. Chagua Kozi na Kampasi

    • Chagua kozi unayotaka kusoma pamoja na kampasi ya TIA unayopendelea kati ya Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Zanzibar, Singida, Kigoma au Mtwara.

  6. Kubali Tamko (Declaration)

    • Soma na thibitisha kuwa taarifa zako ni sahihi kwa kubofya sehemu ya “Declaration”.

  7. Kagua Taarifa Zako na Wasilisha Maombi

    • Tazama kwa makini kila kitu ulichojaza, hakikisha hakuna kosa.

    • Baada ya uhakiki, bonyeza “Submit Application” ili kukamilisha hatua za mwisho.

  8. Pokea Majibu ya Maombi

    • Mfumo wa TIA utakupa mrejesho (feedback) kuhusu maombi yako kupitia akaunti yako ya mtandaoni.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Vigezo vya Kupata Mkopo Ngazi ya Diploma 2025/2026
  2. Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 NECTA ACSEE
  3. Mwisho wa Kutuma Maombi ya Mkopo 2025/2026
  4. Kozi za Diploma Zenye Mkopo 2025/2026
  5. HESLB Yatangaza Kufunguliwa kwa Dirisha la Maombi ya Mikopo 2025/2026
  6. Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 (NECTA Form Six Results)
  7. Tarehe ya Kutangazwa kwa Matokeo ya Kidato cha Sita 2025 na NECTA
  8. Matokeo ya Kidato cha Nne 2024/2025 (NECTA Form Four Results)
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo