Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika 2025/2026 Hatua ya Awali

Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika 2025/2026 Hatua ya Awali

Droo ya mashindano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho msimu wa 2025/2026 imekamilika rasmi leo jijini Dar es Salaam katika makao makuu ya Azam TV.

Ratiba hii imeweka wazi mechi za raundi ya awali, zikishuhudia vilabu vya Tanzania Yanga SC, Simba SC, na Mlandege FC pamoja na Azam FC na Singida Black Stars kwenye Kombe la Shirikisho – vyote vikianza michezo yao katika ugenini.

Tanzania inabaki kuwa miongoni mwa mataifa yanayoendelea kuonesha ushindani mkubwa kwenye soka la Afrika. Kwa sasa, Simba SC inashika nafasi ya tano kwenye chati ya ubora wa klabu za CAF, huku Yanga SC ikishika nafasi ya 12.

Yanga SC – Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wamepangwa dhidi ya washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Angola, Wiliete Benguela, katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

  • Uzoefu wa mashindano: Yanga walifika hatua ya makundi msimu uliopita.
  • Mechi za raundi ya kwanza: Yanga wataanzia ugenini na kumalizia nyumbani.

Kama Yanga itapenya hatua ya kwanza, itakutana na mshindi kati ya Elgeco Plus ya Madagascar au Silver Strikers ya Malawi katika raundi ya pili. Hata katika raundi ya pili, Yanga wataanza ugenini na kumalizia nyumbani – faida muhimu kwa hatua za mtoano.

Simba SC – Mashujaa wa CAF

Washindi wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC, wataanzia ugenini dhidi ya Gaborone United kutoka Botswana.

  • Historia ya CAF: Simba walifika fainali ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita, wakimaliza kama washindi wa pili.
  • Ratiba ya raundi ya kwanza: Mechi ya kwanza ugenini, marudiano nyumbani.
  • Gaborone United: Klabu iliyoanzishwa miaka 58 iliyopita, imewahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Botswana mara 8. Mafanikio yake makubwa kwenye CAF ni kufika raundi ya pili. Jezi zake ni nyekundu na nyeupe.

Iwapo Simba watavuka hatua ya kwanza, watakutana na mshindi kati ya Simba Bhora ya Zimbabwe au Nsingizini Hotspurs ya Eswatini. Hata katika raundi ya pili, Simba wataanza ugenini na kumalizia nyumbani.

Mlandege FC – Wawakilishi wa Zanzibar

Wawakilishi wa Zanzibar, Mlandege FC, wamepangwa dhidi ya Ethiopian Insurance ya Ethiopia.

  • Raundi ya kwanza: Mlandege wataanza ugenini na kumalizia nyumbani.
  • Ikiwa watasonga mbele: watakutana na mshindi kati ya APR ya Rwanda na Pyramids FC ya Misri, ambapo watapangiwa kuanzia nyumbani na kumalizia ugenini.
Mechi Timu ya Nyumbani Timu ya Ugenini
M1,2 Aigle Noir (Burundi) ASAS/Djibouti Télécom (Djibouti)
M3,4 Ethiopian Insurance (Ethiopia) Mlandege FC (Zanzibar)
M5,6 APR FC (Rwanda) Pyramids FC (Misri)
M7,8 Mogadishu CC (Somalia) Kenya Police (Kenya)
M9,10 Jamus FC, Juba (Sudan Kusini) Al Hilal (Sudan)
M11,12 Rahimo FC (Burkina Faso) AS Mangasport (Gabon)
M13,14 Forces Armées (Niger) E.S.T (Tunisia)
M15,16 Dadje FC (Benin) Libya 1
M17,18 ASCK (Togo) RS Berkane (Morocco)
M19,20 East End Lions (Sierra Leone) US Monastirienne (Tunisia)
M21,22 Bibiani Goldstars (Ghana) JS Kabylie (Algeria)
M23,24 Fundacion Bata (Equatorial Guinea) FC Nouadhibou (Mauritania)
M25,26 AS Tempête Stade Malien (Mali)
M27,28 Libya 2 Horoya AC (Guinea)
M29,30 Real De Banjul (Gambia) ASFAR (Morocco)
M31,32 Colombe Sportive (Cameroon) ASC Jaraaf (Senegal)
M33,34 FC Fassell (Liberia) MC Alger (Algeria)
M35,36 Remo Stars (Nigeria) US Zilimadjou (Comoros)
M37,38 Simba Bhora (Zimbabwe) Nsingizini Hotspurs (Eswatini)
M39,40 Gaborone United (Botswana) Simba SC (Tanzania)
M41,42 Elgeco Plus (Madagascar) Silver Strikers (Malawi)
M43,44 Wiliete Benguela (Angola) Yanga SC (Tanzania)
M45,46 Côte d’Or (Seychelles) Stade d’Abidjan (Ivory Coast)
M47,48 Cercle Joachim (Mauritius) Atletico Petroleos (Angola)
M49,50 AC Léopards (Congo Brazzaville) Black Bulls (Mozambique)
M51,52 RD Congo 1 Rivers United (Nigeria)
M53,54 African Stars (Namibia) Vipers SC (Uganda)
M55,56 Power Dynamos (Zambia) ASEC Mimosas (Ivory Coast)
M57,58 RD Congo 2 El Merreikh (Sudan)
M59,60 Llol FC (Equatorial Guinea) Orlando Pirates (Afrika Kusini)

Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika 2025/2026 Hatua ya Awali

Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika 2025/2026 Hatua ya Awali
Ratiba ya Klabu Bingwa Afrika 2025/2026 Hatua ya Awali

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mshahara wa Celestin Ecua Yanga 2025/2026
  2. Msimamo Kundi la Tanzania CHAN 2024
  3. Mohamed Hussein Shabalala Ajiunga na Yanga SC Baada ya Miaka 11 Simba
  4. Ratiba ya CHAN 2025 Mechi za Makundi
  5. Orodha ya Wachezaji Wazawa Yanga Sc 2025/2026
  6. CV Ya Mohamed Doumbia Kiungo Mpya wa Yanga 2025/2026
  7. Cv ya Mohammed Bajaber Kiungo Mshambuliaji Mpya Simba Sc 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo