Tetesi za Usajili simba 2024/2025

Tetesi za Usajili simba 2024/2025 | Wachezaji Waliosajiliwa Simba 2024/2025

Simba ni moja kati ya klabu kongwe nchini Tanzania ambayo yenye historia kubwa na mshabiki wengi Afrika mashariki na kati. Katika historia ya Simba kumekuwako na wachezaji mbalimbali ambao baadhi waliweza kuisaidia klabu hii kuandika historia yenye mafanikio makubwa kwa kutwaa makombe na kufuzu kushiriki michuano ya soka la ushindani barani Afrika.

Miongoni mwa wachezaji wenye kipaji kikubwa cha kusakata kandanda waliowahi chezea klabu ya Simba sc ni Emmanuel okwi, Juma Kaseja, John Bocco, Jonas mkude, Muhhamed Hussein na wengineo wengi.

Hata hivyo, msimu wa 2023/2024 ulikuwa mgumu kwa Simba SC, kwani walimaliza ligi kuu katika nafasi ya tatu, hivyo kukosa nafasi ya kushiriki katika michuano ya klabu bingwa Afrika (CAF). Mafanikio yao yalikuwa tu kushinda Ngao ya Jamii na Kombe la Muungano, huku wapinzani wao wakubwa, Yanga, wakibeba mataji makubwa zaidi, ikiwa ni pamoja na ubingwa wa ligi kuu na Kombe la Shirikisho.

Katika kuimarisha kikosi kuelekea msimu wa 2024/2025 klabu ya Simba sasa ipo sokoni kutafuta wachezaji wapya wenye vipaji vikubwa watakao ipambania jezi nyekundu katika kurudisha heshima ya Simba kwenye michuano mbalimbali. Hapa tutakuletea orodha ya wachezaji wote watakaosajiliwa na simba pamoja na tetesi za usajili za Simba Sc.

Tetesi za Usajili simba 2024/2025

Tetesi za Usajili simba 2024/2025

Msimu wa 2023/24 umekuwa wa changamoto kwa Simba SC, na sasa wameanza kujipanga upya kwa msimu ujao kwa kuingia sokoni kusaka wachezaji wapya wenye vipaji. Tetesi za usajili zimekuwa zikishika kasi, na hapa tunakuletea muhtasari wa kina kuhusu wachezaji wanaotajwa kujiunga na Wekundu wa Msimbazi.

1. Elie Mpanzu – Winga Mpya Kutoka DR Congo

Simba SC inatajwa kumsajili Elie Mpanzu, winga mwenye umri wa miaka 22 kutoka klabu ya AS Vita Club ya DR Congo. Mpanzu ametia saini mkataba wa miaka miwili na anatarajiwa kuongeza kasi na ubunifu katika safu ya ushambuliaji ya Simba.

2. Agostinho Cristóvão Paciência ‘Mabululu’ – Mshambuliaji Kutoka Misri

Simba inatajwa kumnyatia mshambuliaji hatari Agostinho Cristóvão Paciência ‘Mabululu’ kutoka klabu ya Al Ittihad Alexandria ya Misri. Mabululu amekuwa na msimu mzuri nchini Misri, akifunga mabao 10 katika mechi 16 za ligi. Uwepo wake unaweza kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji ya Simba.

3. Mohamed Damaro Camara & Ousmane Fernandez ‘Drame’ – Viungo Kutoka Guinea

Simba inaripotiwa kuwafuatilia kwa karibu viungo wawili wa klabu ya Hafia FC ya Guinea, Mohamed Damaro Camara na Ousmane Fernandez ‘Drame’. Wawili hawa wanaweza kuziba pengo la Sadio Kanoute na Fabrice Ngoma, ambao wanatajwa kuondoka Simba. Uwezo wao katika kucheza nafasi mbalimbali katika kiungo unaweza kuwa msaada mkubwa kwa Simba.

4. Fiston Kalala Mayele – Mshambuliaji Mwenye Uzoefu Kurudi Tanzania?

Tetesi zinadai kuwa Simba imeonyesha nia ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji Fiston Kalala Mayele kutoka klabu ya Pyramids FC ya Misri. Mayele anafahamika sana nchini Tanzania kutokana na kipindi chake cha mafanikio akiwa na Young Africans. Kurudi kwake kunaweza kuongeza uzoefu na uwezo wa kufunga mabao katika kikosi cha Simba.

5. Lameck Lawi – Beki Imara Kutoka Coastal Union

Simba inasemwa imekamilisha usajili wa beki Lameck Lawi kutoka Coastal Union ya Tanga. Lawi anajulikana kwa uwezo wake wa kuzuia mashambulizi na kuanzisha mashambulizi kutoka nyuma. Uwepo wake unaweza kuimarisha safu ya ulinzi ya Simba.

6. Ayoub Lyanga – Kiungo Mshambuliaji Kutoka Azam FC

Simba inatajwa kuwa kwenye mazungumzo na Azam FC kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo mshambuliaji Ayoub Lyanga. Mkataba wa Lyanga na Azam unafikia ukingoni mwa msimu huu, na Simba inaonekana kutaka kumnasa kiungo huyo mwenye kipaji.

7. Fadlu Davids Kuwa Kocha Mpya wa Simba

Kulingana na tetesi, bodi ya Simba imeidhinisha Fadlu Davids kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo kuanzia msimu ujao baada ya mkutano uliofanyika Juni 29. Uvumi wa uamuzi huu unazua maswali kwa baadhi ya watu, kwani Davids alishushwa daraja na Maritzburg msimu uliopita akiwa ligikuu ya Afrika Kusini na kwa sasa anahudumu kama kocha msaidizi katika klabu ya Raja.

Soma Zaidi: Wachezaji Waliosajiliwa Simba 2024/2025

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Tetesi za Usajili Real Madrid 2024/2025
  2. Mshahara wa Kylian Mbappe Real Madrid 2024
  3. Yanga Yafanikiwa Kutetea Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB 2024
  4. Wachezaji wenye Makombe Mengi Ya UEFA
  5. Tetesi Za Usajili Yanga 2024/2025 Transfers Rumors
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo