Rayon Sports vs Yanga Leo 15/08/2025 Saa Ngapi?

Rayon Sports vs Yanga Leo 15/08/2025 Saa Ngapi?

Mashabiki wa soka barani Afrika, hususan Tanzania na Rwanda, leo wanasubiri kwa hamu pambano la kirafiki kati ya Rayon Sports FC na Young Africans SC (Yanga) litakalopigwa kwenye dimba la Amahoro Stadium, jijini Kigali, Rwanda. Mchezo huu ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/2026 kwa upande wa Yanga, lakini pia ni tukio maalum linalojulikana kama Rayon Sports Day 2025 siku ya sherehe kubwa inayoadhimishwa kila mwaka na klabu hiyo maarufu ya nchini Rwanda.

Pambano hili si la kirafiki tu, bali ni kipimo cha nguvu kwa vikosi vyote viwili. Kwa Rayon Sports, hii ni fursa ya kusherehekea historia na mashabiki wao mbele ya wapinzani wakubwa wa ukanda wa Afrika Mashariki.

Kwa upande wa Yanga SC, mchezo huu utatumika kama tathmini muhimu ya kikosi kipya, hasa chini ya kocha mpya ambaye anaendelea kujaribu mbinu na mifumo ya uchezaji kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa mashindano.

Rayon Sports vs Yanga Leo Saa Ngapi?

Kulingana na ratiba rasmi, pambano la Rayon Sports vs Yanga litachezwa leo, tarehe 15 Agosti 2025, katika Uwanja wa Amahoro.

Mchezo utaanza saa 1:00 usiku (19:00) kwa saa za Afrika Mashariki (EAT). Mashabiki wanashauriwa kufika mapema ili kushuhudia burudani mbalimbali zitakazotangulia mchezo, sehemu ya shamrashamra za Rayon Sports Day.

Rayon Sports vs Yanga Leo 15/08/2025 Saa Ngapi?

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ifahamu Gaborone United Wapinzani wa Simba Ligi ya Mabingwa CAF 2025/2026
  2. Makundi ya CHAN 2025 Yatangazwa
  3. Ifahamu Wiliete Benguela Wapinzani wa Yanga CAF 2025/2026
  4. Simba Yatangaza Bei ya Jezi Zao Mpya za 2025-2026
  5. Msimamo wa Makundi CHAN 2025
  6. Ratiba ya Mechi za Leo 12/08/2025 CHAN
  7. Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2025/2026
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo