Yanga Vs CBE SA: Saa Ngapi Mechi Inaanza?
Young Africans SC, maarufu kama Yanga, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wapo tayari kwa mechi yao muhimu ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Commercial Bank of Ethiopia (CBE SA). Mechi hii inatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Abebe Bikila, jijini Addis Ababa.
Saa Ngapi Mechi Inaanza?
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, mechi ya Yanga dhidi ya CBE itaanza saa 09:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Yanga wamefanya maandalizi makali kuelekea mechi hii licha ya changamoto kadhaa. Moja ya changamoto kubwa ni kutokuwepo kwa mchezaji wao nyota, Farid Mussa, ambaye anakosekana kutokana na upasuaji wa nyama za paja (hamstring). Licha ya hilo, kikosi cha Yanga kipo kwenye hali nzuri ya morali, na kocha wao Miguel Gamondi ameonesha imani kubwa kwa wachezaji wake.
Meneja wa Yanga, Walter Harrison, alithibitisha kwamba wachezaji wote waliokuwa kwenye majukumu ya kimataifa wamejiunga na timu jijini Addis Ababa, jambo linaloifanya Yanga kuwa na kikosi thabiti kwa ajili ya mechi dhidi ya CBE.
Harrison alisema: “Tunendelea na mazoezi yetu, na kikosi kipo kwenye hali nzuri. Wachezaji waliohusika kwenye mechi za kufuzu AFCON tayari wamejiunga nasi, na tuko tayari kwa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.”
Aliongeza kuwa, “Morali yetu iko juu, na tuna lengo la kupata matokeo mazuri ugenini, tukijua kuwa tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tunaamini kwenye uwezo wetu.”
Yanga wanakutana na CBE wakiwa na kumbukumbu ya ushindi mkubwa wa jumla ya mabao 10-0 dhidi ya Vital’O FC katika hatua iliyopita. Ushindi huu umewapa Yanga hali ya kujiamini zaidi wanapoelekea katika mechi hii muhimu.
Kikosi cha Yanga kinajumuisha wachezaji wa kimataifa waliorejea baada ya majukumu ya timu zao za taifa. Wachezaji hao ni pamoja na Khalid Aucho kutoka Uganda, Prince Dube wa Zimbabwe, Clatous Chama na Kennedy Musonda kutoka Zambia, Aziz Ki wa Burkina Faso, Djigui Diarra wa Mali, na Duke Abuya kutoka Kenya.
Kwa upande wa Tanzania, wachezaji saba wa Yanga waliteuliwa kuwakilisha Taifa Stars kwenye mechi za kufuzu AFCON. Wachezaji hao ni Mudathir Yahya, Aboutwalib Mshery, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Clement Mzize, na Nickson Kibabage.
Changamoto ya Kukosa Wachezaji Kwenye Mapumziko ya Kimataifa: Licha ya kutokuwepo kwa wachezaji 14 wakati wa mapumziko ya kimataifa, kocha Miguel Gamondi alihakikisha timu inabaki kwenye kasi nzuri kwa kupanga mechi ya kirafiki dhidi ya Kiluvya FC. Yanga walifanikiwa kushinda mechi hiyo kwa mabao 3-0, na kuendelea na maandalizi yao bila matatizo.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Lawi Ndani ya Kikosi cha Coastal Union Dhidi ya Mashujaa
- Kocha wa Kagera Sugar Aelezea Masikitiko Baada ya Vipigo Mfululu
- Wachezaji Simba Waahidi Ushindi Dhidi ya Al Ahly Tripoli
- Coastal Union yamkana Juma Mgunda
- Matokeo ya Coastal Union Vs Mashujaa Leo 13/09/2024
- Kundi la Tanzania Kufuzu AFCON U20 Kanda ya CECAFA
- Ratiba Ngao ya Jamii Wanawake 2024
- Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
Weka Komenti