Cv ya Neo Maema Kiungo Mpya wa Simba 2025/2026

Cv ya Neo Maema Kiungo Mpya wa Simba 2025/2026

Klabu ya Simba SC imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji, Neo Maema, kutoka Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa mkataba wa mwaka mmoja, huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine kulingana na makubaliano. Usajili huu umetangazwa rasmi tarehe 21 Agosti 2025, wakati Simba ikijiandaa kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2025/2026.

Hapa chini tumekuandalia CV kamili ya Neo Maema Kiungo Mpya wa Simba 2025/2026, ikionyesha safari yake ya soka, mafanikio, na matarajio mapya akiwa na Wekundu wa Msimbazi.

Taarifa Binafsi za Neo Maema

  • Jina Kamili: Neo Maema
  • Tarehe ya Kuzaliwa: 1 Desemba 1995
  • Umri: Miaka 29 (2025)
  • Urefu: 1.67m
  • Nchi: Afrika Kusini
  • Mguu Anaotumia: Kushoto
  • Nafasi Uwanjani: Kiungo Mshambuliaji
  • Wakala: JDR Consulting
  • Klabu ya Sasa: Simba SC
  • Alijiunga na Simba: 21 Agosti 2025

Cv ya Neo Maema Kiungo Mpya wa Simba 2025/2026

Neo Maema alianza kutambulika kwenye ligi kuu ya Afrika Kusini kupitia klabu ya Bloemfontein Celtic kabla ya kujiunga na Mamelodi Sundowns mnamo 2021. Akiwa na Sundowns, alijijengea heshima kubwa kutokana na kiwango chake cha juu, akicheza jumla ya michezo 120, kufunga mabao 14 na kutoa asisti 13 katika michuano mbalimbali.

Mafanikio yake na Sundowns ni pamoja na:

  1. Ubingwa wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini mara nne
  2. Kombe la Nedbank Cup mara moja
  3. Kombe la MTN8 mara moja
  4. Taji la African Football League mara moja

Kufikia Agosti 2025, Sundowns ilimuachia rasmi Maema, na Simba SC ikatumia fursa hiyo kumsajili kama sehemu ya maboresho ya kikosi chake kuelekea msimu mpya.

Uzoefu wa Kimataifa

Maema amewahi kuiwakilisha Bafana Bafana, timu ya taifa ya Afrika Kusini, hususan katika mashindano ya CHAN 2024. Katika michuano hiyo, aliteuliwa kuwa nahodha wa timu na akafunga bao moja katika mechi nne alizocheza. Hata hivyo, Bafana Bafana walishindwa kufuzu hatua ya robo fainali baada ya kutoka sare ya 3-3 dhidi ya Uganda.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Wafungaji Bora CHAN 2025
  2. Tanzania Vs Morocco Chan 22/08/2025 Saa Ngapi?
  3. Jonathan Sowah Kuikosa Simba vs Yanga Ngao ya Jamii Septemba 16, 2025
  4. Sherehe za Wiki ya Mwananchi 2025 Yanga Day Kufanyika Benjamin Mkapa Septemba 12
  5. Khalid Aucho Asaini Mkataba wa Miaka 2 na Singida Black Stars
  6. Ratiba ya Robo Fainali CHAN 2025 | Mechi za Robo fainali CHANI
  7. Timu zilizofuzu Robo Fainali CHAN 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo