Ratiba ya Timu ya Taifa ya Tanzania ya Kufuzu Kombe la Dunia 2026
Baada ya kupata sare muhimu ugenini, Taifa Stars inarejea nyumbani kwa ajili ya mchezo mwingine wa hatua ya makundi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026. Jumanne hii macho na masikio ya Watanzania yatakuwa kwenye dimba la Amaan Complex, Zanzibar, ambako Stars itachuana na Niger majira ya saa 10:00 jioni. Mashabiki wataweza kushuhudia mechi hili mubashara kupitia AzamTvMaxApp kwenye chaneli ya ZBC2.
Kwa sasa, Tanzania inashika nafasi ya pili katika Kundi E ikiwa na jumla ya pointi 10. Nafasi hii inaiweka Stars katika mazingira mazuri ya kuendelea kuwania tiketi ya kucheza Kombe la Dunia 2026. Mfumo wa kufuzu unaruhusu timu zitakazoshika nafasi ya pili zenye pointi nyingi zaidi kupenya hadi hatua ya mchujo, jambo linaloongeza matumaini kwa Watanzania.
Mechi Zilizobaki kwa Taifa Stars
Safari ya Stars bado haijaisha. Tanzania imebakiza mechi mbili muhimu dhidi ya Zambia na Niger. Ikiwa itapata ushindi katika michezo hiyo, kikosi cha Stars kitapanda hadi kufikisha pointi 16 – kiwango kinachoweza kuwa msingi wa uhakika kuelekea hatua inayofuata.
Ratiba ya Timu ya Taifa ya Tanzania ya Kufuzu Kombe la Dunia 2026
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply