Azam FC Yawapa Mkono wa Kwaheri Wanne Kwa Mpigo
Wana Rambaramba wa Chamanzi Azam FC leo wametangaza rasmi kuwaaga wachezaji wao wanne wa kigeni waliokuwa sehemu ya kikosi cha msimu uliopita. Hatua hii imechukuliwa ikiwa ni sehemu ya maboresho makubwa ya timu kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Wachezaji Walioachwa
Kwa mujibu wa taarifa za klabu, wachezaji waliokamilisha safari yao na Azam FC ni:
- Jhonier Blanco
- Mamadou Samake
- Franck Tiesse
- Ever Meza
View this post on Instagram
Wachezaji hao walijiunga na Azam kwa matarajio makubwa, lakini baadhi walishindwa kuonyesha kiwango kinachoridhisha uwanjani, huku wengine wakikumbwa na changamoto za majeraha ya mara kwa mara na kushindindwa kuitumika timu kwa muda mrefu. Hali hii imechangia uamuzi wa uongozi kuachana nao mapema kabla ya pazia la msimu mpya kufunguliwa.
Sababu Kuwaaga Nyota Hawa
Azam FC imekuwa moja ya klabu zinazoweka malengo ya kupambana vikali na vigogo wa soka la Tanzania, Simba SC na Yanga SC. Hata hivyo, mara kadhaa safari yao imekuwa ikikwama katika hatua za mwisho za mashindano, jambo lililowalazimu viongozi wa klabu kufanya mabadiliko ya kina ndani ya kikosi. Uamuzi wa kuachana na wachezaji hao wanne unalenga kuongeza ushindani wa ndani ya timu na kuhakikisha kila mchezaji anayepewa nafasi anakuwa na mchango mkubwa kwa mafanikio ya klabu.
Usajili Mpya na Maboresho ya Kikosi
Wakati wakiaga nyota hao, Azam FC tayari imefanya maboresho makubwa ya kikosi chake kuelekea msimu wa 2025/2026 kwa kusajili wachezaji wapya ambao wameongeza matumaini makubwa kwa mashabiki. Hadi sasa, nyota wapya waliokamilisha usajili wao ni:
- Ben Zitoun
- Jephte Kitambala
- Lameck Lawi
- Himid Mao
- Sadio Kanoute
- Pape Doudou
- Barakat Hmidi
- Issa Fofana
Wachezaji hawa wapya wanatarajiwa kuleta ushindani mkubwa ndani ya kikosi na kuongeza nguvu kwa malengo ya klabu kushindana kwenye ligi kuu ya NBC Tanzania na michuano ya kimataifa.
Maboresho ya Azam FC hayakuishia kwenye wachezaji pekee. Klabu hiyo pia ilifanya mabadiliko makubwa kwenye benchi la ufundi, ikimtambulisha kocha mzoefu Florent Ibenge, ambaye alichukua nafasi ya Rachid Taoussi. Ibenge ni jina kubwa barani Afrika, na ujio wake unatarajiwa kuimarisha mbinu na nidhamu ya kikosi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Ngao ya Jamii 2025/2026
- Kikosi cha Yanga 2025/2026 | Wachezaji Wote wa Yanga
- Kikosi cha Timu ya Taifa Wanawake U20 Kilichoitwa Kambini September 2025
- Ratiba ya Mechi za Yanga Ligi Kuu ya NBC 2025/2026
- Ratiba ya Timu ya Taifa ya Tanzania ya Kufuzu Kombe la Dunia 2026
- Ratiba ya NBC Premier league 2025/2026
- Simba yamtambulisha Wilson Nangu
Leave a Reply