Azam Vs Simba Leo 26/09/2024 Saa Ngapi?
Leo tarehe 26 Septemba 2024, mashabiki wa kandanda Tanzania wanatarajia kushuhudia moja ya michezo mikubwa zaidi kwenye Ligi Kuu ya NBC, ambapo wana rambaramba Azam FC watawakalibisha wekundu wa msimbazi Simba SC. Mchezo huu utapigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, majira ya saa 2:30 usiku, na unatarajiwa kuwa na ushindani wa aina yake.
Ushindani wa Azam na Simba
Mara nyingi, mechi baina ya Azam na Simba huwa na mvuto wa kipekee kutokana na kiwango cha soka kinachoonyeshwa na wachezaji wao. Simba, inayoshiriki michuano ya kimataifa ya CAF, inakuja na kikosi chenye uzoefu wa kutosha, huku ikiwa na ushindi wa mechi kadhaa za kimataifa. Kikosi cha Simba kinaundwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa kama Yusuph Kagoma, Jean Charles Ahua, na mshambuliaji nyota Debora Mavambo, ambaye amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu.
Upande wa Azam, wapo mastaa kama Feisal Salum ‘Fei Toto’, Adolf Mtasingwa, na James Akaminko ambao wamekuwa wakitamba kwa soka safi. Hata hivyo, changamoto kwa Azam imekuwa ni kupata matokeo thabiti, kwani licha ya kucheza soka la kuvutia, mara kadhaa wamejikuta wakipoteza au kutoka sare.
Rekodi ya Mechi Baina ya Timu Hizi
Katika historia ya ligi, timu hizi mbili zimekutana mara 32 tangu Azam ilipopanda Ligi Kuu mwaka 2008. Kati ya mechi hizo, Simba imeibuka na ushindi mara 14, huku Azam wakishinda mara 6 tu. Mechi 12 kati ya hizo ziliisha kwa sare. Simba pia imeongoza kwa idadi ya mabao, ikifunga mabao 44 dhidi ya 29 ya Azam.
Simba imekuwa mbabe kwenye michezo dhidi ya Azam, hasa kwenye michezo iliyochezwa ugenini. Hadi sasa, timu hizo zimekutana mara mbili nje ya Dar es Salaam, na pambano la leo linakuwa la tatu. Katika mchezo wa mwisho nje ya Dar, Simba ilitoka sare ya 1-1 na Azam katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mapendekezo ya Mhariri:
Weka Komenti