Bao la Dakika za Jioni Dhidi ya Burnley Lairudisha Liverpool kileleni EPL

Bao la Dakika za Jioni Dhidi ya Burnley Lairudisha Liverpool kileleni EPL

Bao la mkwaju wa penalti uliopigwa na Mohamed Salah katika dakika za majeruhi, Jumapili Septemba 14, 2025, limeipa Liverpool pointi tatu muhimu ugenini dhidi ya Burnley na kuirudisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England (EPL). Penalti hiyo ilitolewa na refa Michael Oliver baada ya Hannibal Mejbri wa Burnley kushika mpira katika eneo la hatari akijaribu kuzuia krosi ya Andrew Robertson. Ushindi huo umeifanya Liverpool kufikisha pointi 12, ikiipiku Arsenal iliyo nafasi ya pili ikiwa na pointi 9.

Burnley walikumbana na pigo dakika ya 84 baada ya Lesley Ugochukwu kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia kadi ya pili ya njano, hali iliyoacha pengo kubwa katika safu ya ulinzi na kurahisisha mashambulizi ya wageni.

Bao la Dakika za Jioni Dhidi ya Burnley Lairudisha Liverpool kileleni EPL

Rekodi Mpya kwa Liverpool

Ushindi huu ulihakikisha Liverpool inaweka rekodi ya kipekee msimu huu: kushinda michezo yote minne ya kwanza ya EPL kupitia mabao yaliyopatikana ndani ya dakika 10 za mwisho. Hii ni mara ya tatu katika historia ya klabu hiyo kufanya hivyo katika michezo minne ya kwanza, mara mbili za awali zikiwa misimu ya 2018/2019 na 2019/2020.

Bao la dakika za jioni dhidi ya Burnley pia limeifanya Liverpool kufikisha mabao 47 yaliyofungwa baada ya dakika ya 90 katika historia ya EPL rekodi inayothibitisha tabia ya kikosi cha Arne Slot kupigania ushindi hadi sekunde za mwisho.

Salah Aendelea Kuthibitisha Ubora Wake

Mohamed Salah aliandika historia nyingine kwa kufikisha mabao 188 ya EPL, akipanda hadi nafasi ya nne kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa ligi hiyo. Mkwaju wake wa penalti katika muda wa nyongeza ulionyesha utulivu na uzoefu mkubwa wa mshambuliaji huyo, akiendeleza nafasi yake kama mchezaji muhimu zaidi wa Liverpool katika mechi za awali za msimu huu.

Burnley Yapoteza Rekodi ya Kudumu Bila Kufungwa

Kichapo hicho kimehitimisha rekodi ya Burnley ya michezo 24 bila kupoteza katika EPL, rekodi iliyojumuisha ushindi 15 na sare tisa. Timu hiyo pia imeweka rekodi nyingine isiyopendeza: kuwa klabu ya kwanza kupoteza michezo miwili mfululizo ya ligi kwa kuruhusu penalti baada ya dakika 90.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kelvin John Aendeleza Moto Baada ya Kuifungia Aalborg Goli 2 Wakiilaza Middelfart 4-0
  2. Msimamo Ligi Kuu Ujerumani Bundesliga 2025/2026
  3. Juventus Yaicharaza Inter Milan 4-3 Ligi Kuu Italia
  4. Singida BS Yatinga Fainali ya CECAFA Kagame Cup Baada ya Kuifunga KMC 2-0
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo