Simba vs Fountain Gate Leo 25/09/2025 Saa Ngapi?
Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo Alhamisi tarehe 25 Septemba 2025 wanatarajiwa kushuka dimbani katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kuivaa Fountain Gate kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2025/2026. Baada ya kushindwa kutamba mbele ya watani wao wa jadi Yanga SC katika misimu kadhaa iliyopita, Simba itaingia katika mchezo huu wakiwa na shauku kubwa ya kuanza kampeni mpya ya ligi kwa ushindi na kurejesha heshima kwa mashabiki wao.
Saa ngapi mechi ya Simba vs Fountain Gate leo?
Mchezo wa Simba vs Fountain Gate leo 25/09/2025 utapigwa majira ya saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Mashabiki wa soka nchini wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hili linaloashiria mwanzo wa safari mpya kwa upande wa Simba, huku Fountain Gate wakitafuta nafasi ya kuandika historia.
Maandalizi na Kauli za Makocha
Simba SC
Kocha Matola amesema:
“Tupo tayari na tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi tatu katika mchezo huu wa kwanza wa ligi. Malengo yetu ni kuchukua ubingwa wa msimu huu, hivyo lazima tuanze vizuri.”
Aidha, ameonya mashabiki kutarajia mchezo mgumu kutokana na hali ya wapinzani wao waliopoteza mechi ya kwanza na watakaotaka kujipatia matokeo chanya ili kurejesha morali.
Fountain Gate
Kwa upande wa Fountain Gate, kocha Denis Kitambi amekiri changamoto ya maandalizi kutokana na idadi ndogo ya wachezaji waliopo tayari, lakini amesisitiza kuwa hawatacheza kwa hofu.
“Presha kubwa ipo kwa Simba, si kwetu. Malengo yetu ni kuhakikisha tunatumia nafasi chache tutakazopata na kuonyesha kiwango bora licha ya changamoto zilizopo,” alisema Kitambi.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania 2025/2026
- Matokeo ya Yanga vs Pamba Jiji Leo 24/09/2025
- Vilabu Bora Afrika 2025 (CAF Club Ranking 2025)
- Hat-Trick ya Mayele Yaipa Pyramids Ubingwa wa FIFA African-Asian-Pacific
- Ratiba ya NBC Premier league 2025/2026
- Serikali Yatoa Ufafanuzi Pamba Jiji Kufanya Mazoezi Gizani Uwanja wa Taifa
- Ratiba ya Mechi za Leo 24/09/2025
Leave a Reply