Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier League

Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier League | Msimamo Wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024-2025

Msimu wa 2023/2024 wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania umekamilika kwa kishindo, Yanga SC wakiibuka mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo. Wanajangwani hao walimaliza kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 80 baada ya kucheza mechi 30, wakishinda mechi 26, wakitoa sare mbili, na kupoteza mbili pekee. Azam FC na Simba SC walimaliza nafasi ya pili na ya tatu mtawalia, zote zikiwa na pointi 69, huku Azam FC ikiwazidi Simba kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Msimu wa 2024/2025 unatarajiwa kuwa na mvuto mkubwa zaidi, huku timu zikifanya usajili wa nguvu na kujiandaa kwa ajili ya kuwania taji la ubingwa. Je, Yanga SC wataweza kutetea ubingwa wao?

Azam FC na Simba SC zitaweza kuwashusha Yanga kutoka kileleni? Je, tutashuhudia timu zingine zikiibuka na kuwa miongoni mwa washindani wakuu? Maswali haya na mengine mengi yatajibiwa kadri msimu huu utakavyokuwa ukiendelea.

Mashabiki wa soka Tanzania wana kila sababu ya kutazamia msimu uliojaa msisimko, ushindani mkali, na mshangao mwingi. Ligi Kuu ya NBC 2024/2025 inaahidi kuwa msimu ambao hautakumbukwa tu kwa matokeo yake, bali pia kwa ubora wa soka litakalochezwa.

Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier League

Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 | Msimamo Wa Ligi Kuu Bara 2024-2025

Pos

TimuPWDLGFGAGDPts
1Singida BS651093616
2Simba54101221013
3Fountain Gate74121412213
4Young Africans440080812
5Azam733162412
6Dodoma Jiji72325419
7Mashujaa62314319
8KMC722348-48
9Tabora UTD7223510-58
10JKT Tanzania61413307
11Tanzania Prisons61413307
12Namungo620446-26
13Coastal Union712469-35
14Kagera Sugar711538-54
15KenGold7115410-64
16Pamba Jiji704329-74
  • MP- Michezo Iliyochezwa (Match Played)
  • W- Ushindi (Winsi)
  • D- Sare (Draw)
  • L-Kufungwa (Lose)
  • GF- Magoli Ambayo Timu Imefunga (Goal For)
  • GA- Magoli Ambayo Timu Imefungwa (Goals Against)
  • GD- Tofauti Ya Magoli (Goal Difference)
  • PTS- Jumla Ya Alama (Points)

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Msimamo Wa Makundi Copa America 2024
  2. Msimamo Kundi la Tanzania Kufuzu Kombe La Dunia 2026
  3. Msimamo Makundi ya EURO 2024
  4. Msimamo wa Ligi Kuu ya Zanzibar 2023/2024 PBZ Premier League Table
  5. Msimamo Ligi ya Vijana Ya NBC U20 Premier League 2023/2024
  6. Msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania 2023/2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo