Matokeo ya Silver Strikers vs Yanga SC Leo 18/10/2025

Matokeo ya Silver Strikers vs Yanga SC Leo 18/10/2025

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania, Yanga SC, leo wanashuka dimbani kwa mara nyingine kupeperusha bendera ya taifa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League). Wanajangwani hao wako nchini Malawi, wakikabiliana na wenyeji Silver Strikers katika mchezo wa raundi ya pili ya hatua za awali ya mashindano hayo.

Mchezo huu wa kukata na shoka unatarajiwa kuchezwa leo Jumamosi, tarehe 18 Oktoba 2025, majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki (4:00 PM EAT), kwenye Uwanja wa Bingu, jijini Lilongwe.

Mchezo wa Silver Strikers vs Yanga SC leo umepewa uzito mkubwa kutokana na historia na ubora wa timu zote mbili. Kwa upande wa Yanga, timu hiyo ipo katika kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu. Mpaka sasa, haijapoteza mechi yoyote kwenye mashindano yote, ikiwa imeshinda michezo minne na kutoka sare mara moja pekee.

Safu yao ya ulinzi imara, ikiongozwa na Djigui Diarra golini pamoja na mabeki wa kati Ibrahim Bacca na Dickson Job, haijaruhusu bao hata moja. Katika upande wa ushambuliaji, Yanga imefunga mabao tisa (9) tangu msimu uanze, ikionyesha makali makubwa ya safu ya mbele.

Katika raundi ya kwanza ya michuano hii ya CAF Champions League, Yanga iliiondoa Wiliete SC ya Angola kwa jumla ya mabao 5–0, ikishinda 3–0 ugenini na 2–0 nyumbani, matokeo yaliyodhihirisha uimara na ubora wa kikosi cha Wanajangwani.

Kwa upande wa Silver Strikers, wao waliiondoa Elgeco PLUS ya Madagascar kwa faida ya bao la ugenini baada ya kupata matokeo ya 1–1 ugenini na 0–0 nyumbani, na hivyo kufuzu kwa raundi ya pili kwa sheria ya bao la ugenini.

Matokeo ya Silver Strikers vs Yanga SC Leo 18/10/2025

Fuatilia Hapa Matokeo ya Silver Strikers vs Yanga SC Leo 18/10/2025

Timu Timu
Silver Strikers 🇲🇼 VS Yanga SC 🇹🇿
🏆 #CAFCL 2nd Preliminary Round – 1st Leg
📅 Tarehe: 18 Oktoba 2025
🏟️ Uwanja: Bingu National Stadium, Lilongwe
Muda: 4:00 PM 🇹🇿 / 3:00 PM 🇲🇼

Matokeo ya moja kwa moja yatapatikana hapa pindi mchezo utakapoanza. Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa taarifa kamili kuhusu Matokeo ya Silver Strikers vs Yanga SC Leo 18/10/2025.

Vita ya Kihistoria Kati ya Silver Strikers na Yanga SC

Mchezo wa Silver Strikers vs Yanga SC leo umepewa uzito mkubwa kutokana na historia na ubora wa timu zote mbili. Kwa upande wa Yanga, timu hiyo ipo katika kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu. Mpaka sasa, haijapoteza mechi yoyote kwenye mashindano yote, ikiwa imeshinda michezo minne na kutoka sare mara moja pekee.

Safu yao ya ulinzi imara, ikiongozwa na Djigui Diarra golini pamoja na mabeki wa kati Ibrahim Bacca na Dickson Job, haijaruhusu bao hata moja. Katika upande wa ushambuliaji, Yanga imefunga mabao tisa (9) tangu msimu uanze, ikionyesha makali makubwa ya safu ya mbele.

Katika raundi ya kwanza ya michuano hii ya CAF Champions League, Yanga iliiondoa Wiliete SC ya Angola kwa jumla ya mabao 5–0, ikishinda 3–0 ugenini na 2–0 nyumbani, matokeo yaliyodhihirisha uimara na ubora wa kikosi cha Wanajangwani.

Kwa upande wa Silver Strikers, wao waliiondoa Elgeco PLUS ya Madagascar kwa faida ya bao la ugenini baada ya kupata matokeo ya 1–1 ugenini na 0–0 nyumbani, na hivyo kufuzu kwa raundi ya pili kwa sheria ya bao la ugenini.

Kauli ya Kocha Patrick Mabedi – Vita ya Nyumbani

Kocha msaidizi wa Yanga, Patrick Mabedi, ambaye ni raia wa Malawi, ameeleza hisia zake kabla ya mchezo huu, akisema kuwa ni mechi ya kipekee kwake binafsi kwani anarudi nyumbani kucheza dhidi ya timu ya taifa lake.

“Mechi hii ni muhimu sana, ninarudi nyumbani tunakwenda kucheza na Silver Strikers ambayo ni timu ya nyumbani. Tutafanya kile tunachoweza ili kupata matokeo mazuri na kufuzu hatua inayofuata,” alisema Mabedi.

Mabedi pia amefichua kuwa anawafahamu vizuri baadhi ya wachezaji wa Silver Strikers, kwani wakati akiwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Malawi, aliwahi kuwafundisha wachezaji kadhaa waliopandishwa kutoka kikosi cha vijana chini ya miaka 20.

“Kucheza na timu yenye wachezaji unaowafahamu ni faida kubwa. Ninajua udhaifu na nguvu zao, lakini mwisho wa yote tunapaswa kupambana ili kupata matokeo mazuri,” aliongeza.

Hata hivyo, kocha huyo alionya wachezaji wake kuwa Silver Strikers si timu ya kubezwa, licha ya kuwa na matokeo yasiyoridhisha katika michezo mitatu iliyopita (sare mbili na kipigo kimoja).

“Katika soka, timu inaweza kuwa haipati matokeo mazuri, lakini ikafanya vizuri dhidi ya timu kubwa. Yanga ni timu kubwa, hivyo wapinzani wetu watacheza kwa nguvu zaidi. Tunapaswa kuwa makini,” alisema Mabedi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Silver Strikers vs Yanga Sc Leo 18/10/2025 Saa Ngapi?
  2. Timu Zilizofuzu Kombe la Dunia 2026
  3. Msimamo wa Ligi Kuu Zanzibar PBZ 2025/2026
  4. Majina Ya Usaili Kusimamia Uchaguzi 2025 Jimbo La Temeke, Mbagala na Chamazi
  5. Pacome Anukia Kombe la Dunia Baada ya Ushindi 7-0 Dhidi ya Shelisheli
  6. Zimbabwe Yainyima Nafasi Afrika Kusini Kufuzu Kombe la Dunia
  7. Kaizer Chiefs Ya Thibitisha Kuachana na Kocha Nasreddine Nabi
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo