Mahitaji ya Kwenda Nayo Kambi JKT | Vitu vya Kwenda Navyo JKT Mujubu Wa Sheria | Vitu vya Kuripoti navyo JKT
Tarehe 24 Ya Mwezi wa tano mwaka huu 2024 Jeshi la kujenga Taifa JKT lilitangaza majina ya wanafunzi waliohitimu kidato cha Sita ambao wanatakiwa kuripoti katika makambi mbalimbali ya JKT kwa ajili ya Mafunzo ya JKT mujibu wa sheria. Maelfu ya wahitimu wa kidato cha sita wamepangiwa kujiunga katika makambi mbalimbali yaliopo mikoa tofauti Tanzania.
Aidha, JKT limetoa nyongeza ya awamu ya pili ya majina ya Vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwaka 2024 kujiunga na JKT ili kufanya mafunzo hayo ya Lazima. Vijana hao, waripoti katika Makambi ya JKT yaliyo karibu na mahali wanapoishi. Vijana hao wote wanatakiwa kuripoti Makambini kuanzia tarehe 22 Juni 2024 hadi tarehe 26 Juni 2024.
Vifaa vinavyohitajika Kwa Vijana wa Kujiunga na Mafunzo ya )KT kwa Mujibu wa Sheria 2024 ni kama vifuatavyo
- Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni, iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
- T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest).
- Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
- Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
- Soksi ndefu za rangi nyeusi.
- Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
- Track suit ya rangi ya kijani au blue.
- Nyaraka zote zinazohitajika katika Udahili wa Kujiunga na Elimu ya Juu, zikiwemo cheti vya Kuzaliwa, Vyeti vya Kuhitimu kidato cha Nne nk.
- Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.
Mapendekezo Ya Mhariri:
Weka Komenti