Bodi ya Mikopo HESLB Yatangaza Awamu ya Kwanza ya Wanafunzi Waliopata Mkopo 2025/2026
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Ijumaa, Oktoba 24, 2025, imetangaza awamu ya kwanza ya upangaji wa mikopo na ruzuku kwa mwaka wa masomo 2025/2026, ambapo jumla ya wanafunzi 135,240 wamepata mikopo na ruzuku kwa ajili ya kugharamia masomo yao katika vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu nchini.
Katika awamu hii, HESLB imetoa jumla ya fedha zote zenye thamani ya TZS bilioni 426.5, zikigawanywa kwa makundi yafuatayo:
- Wanafunzi 40,952 wa shahada ya awali na wanafunzi 5,342 wa stashahada wamepangiwa mikopo yenye jumla ya TZS bilioni 152.
- Wanafunzi 615 wa Samia Scholarship wamepangiwa ruzuku yenye thamani ya TZS bilioni 3.3.
- Wanafunzi 88,331 wanaoendelea na masomo wamepangiwa mikopo yenye jumla ya TZS bilioni 271.2, baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka uliopita.
HESLB imesisitiza kuwa itatoa awamu nyingine za mikopo na ruzuku mara tu itakapopokea uthibitisho wa udahili wa wanafunzi wapya na matokeo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, waombaji wote wa mikopo wanakumbushwa kuendelea kufuatilia taarifa za maombi yao kupitia mfumo wa SIPA (Student’s Individual Permanent Account) hadi taratibu zote za uchambuzi na upangaji zitakapokamilika.
Jinsi ya Kuangalia Kama Umepata Mkopo wa HESLB Kupitia Akaunti ya SIPA
Bodi ya Mikopo (HESLB) inatumia mfumo rasmi wa SIPA kama njia pekee ya kuwasiliana na waombaji wa mikopo. Kupitia akaunti hii, mwanafunzi anaweza kupata taarifa zote muhimu kuhusu hali ya maombi yake, ikiwa ni pamoja na kujua kama ameidhinishwa kupata mkopo katika awamu ya kwanza ya wanafunzi waliopata mkopo 2025/2026.
Hatua za Kuangalia Mkopo Kupitia Mfumo wa SIPA
- Fungua tovuti rasmi ya HESLB: Tembelea tovuti rasmi ya Bodi ya Mikopo kupitia kiungo: https://olas.heslb.go.tz/olams/account/login
- Ingia kwenye akaunti yako ya SIPA: Tumia username na password ulizounda wakati wa kujisajili. Hakikisha taarifa hizi zimehifadhiwa kwa usalama ili kuepuka changamoto wakati wa kuingia.
- Fungua sehemu ya “SIPA” kisha chagua “ALLOCATION”: Baada ya kuingia, bofya sehemu ya SIPA, kisha nenda kwenye kipengele cha Allocation ili kufuatilia matokeo ya upangaji wa mkopo wako.
- Chagua mwaka wa masomo 2025/2026: Mfumo utakuelekeza kuchagua mwaka wa masomo husika. Hapa ndipo utapata kuona iwapo maombi yako yameidhinishwa na kiwango cha mkopo kilichotolewa.
- Angalia taarifa za mkopo wako: Ndani ya akaunti yako, utaona taarifa rasmi kutoka HESLB zikionyesha hali ya maombi yako. Ikiwa umefanikiwa kupata mkopo, kiasi cha fedha kilichotolewa kitaoneshwa moja kwa moja, pamoja na mgawanyo wa ada na posho.
Soma Machapisho Mengine
- Majina ya Waliopata Mkopo 2025/2026 HESLB
- NECTA Standard Seven Results 2025: Updates on PSLE Results for All Regions in Tanzania
- Matokeo ya Darasa la Saba 2025 (PSLE)
- Jinsi ya Kuangalia kama Umepata Mkopo wa HESLB 2025/2026
- Matokeo ya Kidato cha Nne 2024/2025 (NECTA Form Four Results)
- Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mkoa wa Kilimanjaro
- Matokeo ya Darasa la Saba 2025 Mkoa wa Arusha









Leave a Reply