Sifa za Kuchaguliwa Kidato cha Kwanza 2025/2026

Sifa za Kuchaguliwa Kidato cha Kwanza 2025/2026

Kuchaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya serikali ni ndoto kubwa kwa kila mwanafunzi au familia ya mwanafunzi aliyehitimu elimu ya msingi. Hii ni kwa sababu shule hizi zinatambulika kwa kutoa elimu bora yenye viwango vya kitaifa, huku zikigharimu ada nafuu au kutokuwa na ada kabisa. Hali hii inazifanya shule za serikali kuwa chaguo kuu kwa wazazi wengi nchini, hususan wale kutoka familia zenye kipato cha chini. Hata hivyo, kutokana na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba kila mwaka na upungufu wa nafasi katika shule za sekondari za serikali, si kila mwanafunzi anaweza kuchaguliwa.

Kwa mujibu wa TAMISEMI, mchakato wa Vigezo vya Kuchaguliwa Kidato cha Kwanza 2025/2026 unazingatia viwango vya ufaulu, uwiano wa nafasi kitaifa, pamoja na mahitaji maalum ya wanafunzi. Makala hii inaeleza kwa kina vigezo hivyo muhimu vinavyotumika katika uteuzi wa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza nchini Tanzania.

Sifa za Kuchaguliwa Kidato cha Kwanza 2025/2026

1. Kiwango cha Alama za Ufaulu

Kigezo cha kwanza na cha msingi kinachotumika na TAMISEMI ni kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi katika Mtihani wa Kumaliza Darasa la Saba (PSLE). Ili mwanafunzi achaguliwe kuendelea na elimu ya sekondari katika shule za serikali, ni sharti awe amepata alama kati ya 121 hadi 300 kati ya alama 300. Hii ndiyo kiwango kinachotambuliwa rasmi kama ufaulu wa kuridhisha unaoonyesha uwezo wa mwanafunzi kuendelea na masomo ya sekondari.

Kwa kawaida, wanafunzi wenye alama za juu zaidi hupata nafasi katika shule zenye hadhi ya juu zaidi, ikiwa ni pamoja na shule za bweni za kitaifa na zile maalum za ufundi.

2. Mgawanyo wa Nafasi Kitaifa kwa Shule za Sekondari za Bweni za Serikali

Shule za bweni za serikali zinachukuliwa kuwa ni za kitaifa, jambo linalomaanisha kwamba wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga nazo wanatoka katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Mgawanyo huu wa nafasi unalenga kuimarisha umoja wa kitaifa na kuhakikisha usawa wa fursa kwa wanafunzi wote, bila kujali walikotoka.

Shule hizi zimegawanywa katika makundi matatu makuu yafuatayo:

a) Shule za Bweni kwa Wanafunzi Wenye Ufaulu wa Juu Zaidi

Hizi ni shule zenye hadhi ya juu kitaifa zinazojulikana kwa kutoa elimu bora na matokeo mazuri kila mwaka. Miongoni mwa shule hizo ni Msalato, Mzumbe, Kilakala, Kibaha, Ilboru, Tabora Wasichana, na Tabora Wavulana.

Nafasi katika shule hizi zinatolewa kwa wanafunzi waliopata alama za juu zaidi kitaifa. TAMISEMI inagawa nafasi hizo kwa kuzingatia idadi ya watahiniwa waliofanya mtihani katika kila mkoa, huku halmashauri zote ndani ya mkoa zikipewa fursa sawa bila kujali idadi ya watahiniwa. Mfumo huu unalenga kudumisha usawa na kutoa nafasi kwa kila mkoa kushiriki katika shule bora za bweni.

b) Shule za Sekondari za Bweni za Ufundi

Kundi la pili linajumuisha shule zinazotoa elimu maalum ya ufundi na sayansi ya vitendo. Hizi shule zinalenga kuandaa wanafunzi wenye vipaji vya kiufundi na ubunifu. Mgawanyo wa nafasi kwa shule za aina hii hufanywa kwa uwiano sawa katika kila mkoa, kulingana na idadi ya watahiniwa wa darasa la saba.

Lengo kuu la mpangilio huu ni kuhakikisha kwamba wanafunzi kutoka mikoa yote wanapata nafasi sawa ya kupata elimu ya kiufundi, bila kujali hali ya kiuchumi ya eneo wanaloishi.

c) Shule za Bweni za Kawaida

Shule hizi zinalenga kutoa fursa kwa wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu au familia zenye kipato cha chini. Wanafunzi wanaoishi vijijini, yatima, au wanaotoka kwenye halmashauri zenye changamoto za kiuchumi, wanapewa kipaumbele maalum katika kundi hili. Wanafunzi kutoka halmashauri za majiji, manispaa, na miji kwa kawaida hawajumuishwi kwenye kundi hili, isipokuwa wale wenye mahitaji maalum kama ulemavu au changamoto za kiafya.

3. Uhitaji Maalum na Mazingira Magumu

Serikali ya Tanzania kupitia TAMISEMI pia inatilia mkazo haki ya elimu kwa kila mtoto, ikiwemo wale wenye ulemavu au changamoto za kiafya. Wanafunzi hawa wanapewa nafasi maalum katika shule za sekondari za serikali ili kuhakikisha wanapata elimu kwa usawa kama wenzao.

Vilevile, wanafunzi wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto yatima au wale wanaotoka katika mazingira magumu hupatiwa kipaumbele cha pekee wakati wa kugawa nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. NECTA Standard Seven Results 2025: Updates on PSLE Results for All Regions in Tanzania
  2. Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2025/2026 NECTA
  3. Bodi ya Mikopo HESLB Yatangaza Awamu ya Kwanza ya Wanafunzi Waliopata Mkopo 2025/2026
  4. Majina ya Waliopata Mkopo 2025/2026 HESLB
  5. Mambo 5 ya Muhimu Kujua Wakati Wa Kusubiri Kutangazwa kwa Matokeo ya Darasa la Saba 2025
  6. Matokeo ya Darasa la Saba 2025 (PSLE)
  7. Jinsi ya Kuangalia kama Umepata Mkopo wa HESLB 2025/2026
  8. Matokeo ya Kidato cha Nne 2024/2025 (NECTA Form Four Results)
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo