Azam vs Wydad Ac Leo 28/11/2025 Saa Ngapi?

Azam vs Wydad Ac Leo 28/11/2025 Saa Ngapi?

Leo matajiri wa jiji, Azam FC, wanatarajiwa kushuka dimbani kwenye Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar kuwakaribisha Wydad Casablanca (Wydad AC) katika mchezo muhimu wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika. Mchezo huu wa Kundi B utapigwa kuanzia saa 1:00 usiku, huku matangazo ya moja kwa moja yakitarajiwa kurushwa kupitia AzamSports2HD.

Mashabiki wa soka visiwani Zanzibar wametajwa kuwa sehemu muhimu ya nguvu za timu hiyo, ambapo mashabiki 1,000 wa kwanza wataingia bure, huku viingilio vingine vikiwa VIP shilingi 2,000 na mzunguko shilingi 1,000.

Azam vs Wydad Ac Leo 28/11/2025 Saa Ngapi?

Azam vs Wydad AC Leo Saa Ngapi? – Maelezo Muhimu ya Mchezo

Mchezo kati ya Azam FC vs Wydad AC ni wa pili kwa klabu hiyo ya Tanzania kwenye hatua ya makundi ya TotalEnergies CAF Confederation Cup 2025/2026. Baada ya kufungwa 2-0 kwenye mechi yao ya kwanza dhidi ya Maniema Union huko Kinshasa, Azam wanahitaji ushindi muhimu ili kurejesha matumaini ya kusonga mbele.

Kocha mkuu wa Azam FC, Florent Ibenge, akizungumza Alhamisi, alibainisha kuwa kikosi chake kimejiandaa kwa umakini mkubwa na kinaamini sapoti ya mashabiki wa Zanzibar itakuwa chachu ya matokeo mazuri. Ibenge alisema: “Baada ya kupoteza mechi ya kwanza, tunajua tunahitaji kufanya kazi kwa bidii na kupata matokeo mazuri dhidi ya Wydad.”

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. TFF Yatangaza Kuahirishwa kwa Tuzo za Msimu 2024/2025
  2. Timu Tatu za Tanzania Zashindwa Kung’ara Katika Michezo ya Kwanza ya Makundi CAF
  3. Msimamo wa Makundi Kombe la Shirikisho CAF 2025/2026
  4. Msimamo Kundi la Simba Klabu Bingwa 2025/2026
  5. Matokeo ya Simba vs Petro De Luanda leo 23/11/2025
  6. Wachezaji Wanaowania Tuzo za TFF 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo