Kikosi cha Simba Vs Al Ahli Tripoli Leo 22/09/2024 | Kikosi cha Simba Leo Vs Al Ahli Kombe la Shirikisho CAF
Leo, Simba SC itakuwa ikiwakilisha taifa katika mechi ya marudiano ya hatua ya kufuzu makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya. Mechi hii itafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni. Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote ili kufuzu baada ya mchezo wa kwanza kule Libya kumalizika kwa sare ya 0-0.
Simba inaingia kwenye mechi hii kwa morali ya juu, ikiwa imedhamiria kushinda na kufuzu kwa hatua ya makundi kwa mara ya tano mfululizo katika michuano ya klabu barani Afrika. Kocha wa Simba, Fadlu Davids, ameweka wazi kwamba hakuna kingine wanachokitarajia leo zaidi ya ushindi. “Malengo yetu ni kushinda na kufuzu,” alisema Davids wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Kikosi cha Simba kimekuwa kikiimarika kadri msimu unavyoendelea, hasa katika safu ya ulinzi. Katika michezo mitano ya mwisho, Simba imeruhusu bao moja pekee, ikiwapa mashabiki matumaini kuwa wanaweza kudhibiti mashambulizi ya Al Ahli Tripoli.
Licha ya kuonyesha uimara wa safu ya ulinzi, Simba inahitaji kuongeza ubora katika safu ya ushambuliaji. Katika mechi ya awali dhidi ya Al Ahli, Simba ilitengeneza nafasi chache za wazi na haikufanikiwa kupiga shuti lolote lililolenga goli. Mawinga wa timu, Joshua Mutale na Edwin Balua, wanatakiwa kuwa na ufanisi mkubwa leo katika kupenyeza mipira kwa washambuliaji ili kupata mabao ya ushindi.
Pia, Simba itakosa huduma ya kiungo wake muhimu, Mzamiru Yassin, anayesumbuliwa na majeraha ya mguu, ingawa kocha Davids anaamini wachezaji waliobaki wataweza kufidia pengo hilo.
Kikosi cha Simba Vs Al Ahli Tripoli Leo 22/09/2024
Kocha wa Simba Faldu Davis anatarajiwa kutangaza kikosi cha Simba vs Al Ahli Tripoli leo majina ya saa tisa jioni. Mashabiki na wadau wa soka wanataria kuona Davis anakuja na kikosi bora hasa chenye washambuliaji wengi tofauti na kile kilichocheza mechi ya kwanza jijini Tripoli ambacho kilikua na lengo la kuzui mashambilizi ya Al Ahli.
Hapa Habariforum tutakuletea orodha ya wachezaji watakaounda kikosi cha Simba leo kitakacho anza katika mtanange huu wa kuisaka tiketi ya kufuzu hatua ya makundi shirikisho CAF.
Hiki Apa Kikosi cha Simba Vs Al Ahli Tripoli Leo
Hali ya Al Ahli Tripoli
Al Ahli Tripoli sio timu ya kubezwa, kwani ina rekodi nzuri katika mechi za ugenini. Katika michezo 10 ya kimataifa iliyopita wakiwa ugenini, wamefanikiwa kushinda mara nne na kutoka sare mara mbili. Timu hii pia ina safu nzuri ya mabeki wa pembeni ambao mara nyingi hutengeneza mashambulizi. Simba inatakiwa kuwa makini na kasi ya mabeki hawa ili kuepuka kuruhusu mabao.
Hata hivyo, Al Ahli imeonyesha udhaifu katika safu ya ulinzi kwa kuruhusu mabao matatu katika mechi tano zilizopita, jambo linalotoa fursa kwa Simba kupata ushindi ikiwa watacheza kwa umakini.
Rekodi ya Simba Mechi za Nyumbani
Simba imekuwa na rekodi nzuri ya ushindi inapocheza nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Katika michezo 10 ya kimataifa iliyopita, Simba imeshinda mechi sita, kutoka sare mbili na kupoteza mbili. Ardhi ya nyumbani imekuwa ngome imara kwa Simba, huku ikiwapa wapinzani wakati mgumu wanapokuja kucheza Tanzania.
Mashabiki wa Simba wameombwa kutoa sapoti kubwa kwa timu yao bila kuingilia mchezo vibaya, hasa kutokana na vurugu zilizotokea kwenye mechi ya awali nchini Libya. Kocha Fadlu Davids amewaomba mashabiki kuwa watulivu na kuipa timu sapoti stahiki ili waweze kupata matokeo chanya.
Matokeo Yanayotarajiwa
Katika mechi hii, ushindi wowote utaipeleka Simba kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, ambapo watapata kitita cha Dola 100,000 kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Endapo mechi itaisha kwa sare ya mabao, Al Ahli Tripoli watasonga mbele kwa kanuni ya mabao ya ugenini. Iwapo itakuwa suluhu tena, mshindi atapatikana kwa mikwaju ya penalti.
Simba inahitaji kuwa na nidhamu ya hali ya juu na kutumia mbinu zao vizuri ili kupata matokeo mazuri. Ushindi leo sio tu utawapa tiketi ya makundi, bali pia utawapa nafasi ya kuendelea kuwania taji ambalo kwa sasa linashikiliwa na Zamalek ya Misri.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Simba VS AL Ahli Tripoli Leo 22/09/2024 Saa Ngapi
- Timu zilizofuzu Makundi Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
- Matokeo ya Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024
- Yanga Vs CBE SA Leo 21/09/2024 Saa Ngapi
- Kikosi cha Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024
- Ley Matampi Ajitoa Mapema Mbio za Kipa Bora
- Picha za Jezi Mpya za Pamba Fc 2024/2025
Weka Komenti